Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Aprili 2020 07:43:40
Meloxicam
Ni dawa kwa ajili ya kutuliza maumivu makali ya mwili na maungio kwa kupunguza kiwango cha homoni inayoleta madhara hayo mwilini. Dawa hipo kwenye kundi la dawa jamii NSAIDS.
Meloxicam hufanya kazi kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa huambatana na homa Pamoja na uvimbe sehemu yenye shida.
Rangi na fomu ya Meloxicam
Hupatikana mfumo wa vidonge, tembe na maji
Umetaboli wa dawa
Dawa inapoingia mwilini huvunjwa na Ini na sumu yake hutolewa Utoaji taka mwili kupitia Figo kwa njia ya mkojo na kinyesi
Matumizi ya Meloxicam
Kutuliza maumivu ya mwili
Homa
Kupunguza uvimbe
Kutibu maumivu ya athraitis na osteoarthraitizi
Maudhi madogo ya Meloxicam
Kuharisha
Michefuchefu na kutapika
Kuvimbiwa
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Upele
Masikio kupiga kelele
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya chakula
Kuvimba Uso
Kutokwa jasho jingi
Tahadhari ya Meloxicam
Wenye shida ya Figo
Wenye matatizo ya Moyo
Wenye shida ya Ini
Wenye mzio wa Naproxen na dawa zingine
Wenye vidonda vya tumbo(itumike pamoja na antiasidi kuzuia madhara endapo kuna ulazia wa kutumika)
Wenye pumu (asthma)
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Meloxicam
Dawa hii hairuhusiwi kutumika pamoja na
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen, naproxen hii hupelekea hatari ya kupata vidonda vya tumbo
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa zinazozuia damu kuganda mfano warfarin
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya steroids mfano Prednisone
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa methotrexate
Usitumie dawa hii pamoja na Dawa Lithium
Usitumie dawa hii pamoja na Dawa fluoxetine, fluvoxamine
Matumizi ya Meloxicam kwa Wajawazito na Wanaonyonyesha
Kwa Wajawazito
Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi ya mwanzoni na miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.
Kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha kwa sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Je endapo umesahau dozi ya Meloxicam ufanyeje?
Kama umesaau kunywa dose yako unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, acha dozi uliyoruka na kunywa dozi ingine kwa muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
20 Septemba 2023 17:42:09
Rejea za mada hii:-