top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Novemba 2021, 17:38:48

Metronidazole

Metronidazole

Metronidazole ni dawa jamii ya nitroimidazole yenye uwezo wa kuua bakteria jamii ya anaerobic, hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na vimelea wanaodhurika na dawa hii.

Majina ya kibiashara

​

Metronidazole hufahamika kwa majina mengine ya kiboashara kama;


  • Flagyl

  • Flagyl ER

  • Flagyl IV RTU

​

Rangi ya dawa ni ipi?


Rangi ya dawa inatofautiana kuligana na kiwanda, huweza kuwa ya rangi ya njano, nyeupe, brown, bluu n.k

​

Dozi na matumizi


Dozi huweza kupatikana kwa mfumo wa

  • Tembe ya miligramu 375

  • Kidonge cha miligramu 200 na 250, 750

  • Dripu ya miligramu 500 kwa kila mililita 100

Metronidazole hutibu nini?


Metronidazole hutumika yenyewe au pamoja na dawa zingine katika matibabu ya;


  • Maambukizi ya bakteria wa anaerobiki

  • Magonjwa ya zinaa ikitumiwa na dawa zingine

  • Vaginosis ya bakteria

  • Maambukizi baada ya upasuaji wa colorekto

  • Maambukizi ya trichomoniasis

  • Maambukizi ya amoebiasis

  • Maambukizi ya gardinela

  • Maambukizi ya Helikobakter pairoli

  • Urethritis isiyo ya kisonono

  • Magonjwa ya michomo kwenye ndani ya oganiza nyonga kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa

​

Angalizo la dozi ya metronidazole


Dozi inatakiwa rekebishwa kwa wagonjwa wafuatao

Mwingiliano na dawa zingine

​

Metronidazolehairuhusiwi kutumika kabisa pamoja na dawa hizi hapa


  • Dronabinol

  • Flibanserin

  • Lomitapide

​

Metronidazole ikitumika na hizi zinaweza kuleta mdhara makubwa


  • Avapritinib

  • Axitinib

  • Bcg vaccine live

  • Bosutinib

  • Cholera vaccine

  • Cobimetinib

  • Dihydroergotamine

  • Dihydroergotamine intranasal

  • Disulfiram

  • Dronedarone

  • Eliglustat

  • Entrectinib

  • Ergotamine

  • Erythromycin base

  • Erythromycin ethylsuccinate

  • Erythromycin lactobionate

  • Erythromycin stearate

  • Everolimus

  • Fentanyl

  • Fentanyl intranasal

  • Fentanyl transdermal

  • Fentanyl transmucosal

  • Ivabradine

  • Lemborexant

  • Lovastatin

  • Mebendazole

  • Midazolam intranasal

  • Naloxegol

  • Neratinib

  • Olaparib

  • Pimozide

  • Propylene glycol

  • Ranolazine

  • Silodosin

  • Simvastatin

  • Siponimod

  • Sirolimus

  • Tazemetostat

  • Tolvaptan

  • Typhoid vaccine live

  • Venetoclax

  • Warfarin


Metronidazole ikitumika na dawa zifuatazo mgonjwa anatakiwa kuangaliwa kwa karibu ili kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza;


  • Acalabrutinib

  • Alitretinoin

  • Almotriptan

  • Alprazolam

  • Amifampridine

  • Amiodarone

  • Aprepitant

  • Aripiprazole

  • Artemether/lumefantrine

  • Atorvastatin

  • Avanafil

  • Bazedoxifene/conjugated estrogens

  • Bortezomib

  • Brexpiprazole

  • Budesonide

  • Buprenorphine subdermal implant

  • Buprenorphine, long-acting injection

  • Buspirone

  • Cabozantinib

  • Cannabidiol

  • Carbamazepine

  • Carvedilol

  • Cholestyramine

  • Cilostazol

  • Cinacalcet

  • Clobetasone

  • Clopidogrel

  • Clozapine

  • Conivaptan

  • Conjugated estrogens

  • Conjugated estrogens, vaginal

  • Cortisone

  • Cyclosporine

  • Darifenacin

  • Darunavir

  • Dasatinib

  • Deflazacort

  • Dexamethasone

  • Diazepam

  • Diazepam intranasal

  • Digoxin

  • Eletriptan

  • Erlotinib

  • Estradiol

  • Estrogens conjugated synthetic

  • Estropipate

  • Ethanol

  • Ethinylestradiol

  • Ethotoin

  • Etonogestrel

  • Etravirine

  • Felodipine

  • Fesoterodine

  • Fludrocortisone

  • Fluorouracil

  • Fosamprenavir

  • Fosphenytoin

  • Guanfacine

  • Hydrocortisone

  • Hydroxyprogesterone caproate

  • Ibrutinib

  • Ifosfamide

  • Iloperidone

  • Indinavir

  • Isoniazid

  • Ivacaftor

  • Ivosidenib

  • Ixabepilone

  • Lapatinib

  • Levamlodipine

  • Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate

  • Lopinavir

  • Loratadine

  • Losartan

  • Lumefantrine

  • Maraviroc

  • Mefloquine

  • Mestranol

  • Methadone

  • Methylprednisolone

  • Midazolam

  • Naldemedine

  • Nateglinide

  • Nelfinavir

  • Nicardipine

  • Nilotinib

  • Nisoldipine

  • Palbociclib

  • Parecoxib

  • Pazopanib

  • Phenytoin

  • Prednisolone

  • Prednisone

  • Quetiapine

  • Quinidine

  • Repaglinide

  • Rimegepant

  • Ritonavir

  • Ruxolitinib

  • Saquinavir

  • Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid

  • Solifenacin

  • Sonidegib

  • Sufentanil sl

  • Sulfamethoxazole

  • Sunitinib

  • Suvorexant

  • Tacrolimus

  • Tadalafil

  • Tamoxifen

  • Tamsulosin

  • Temsirolimus

  • Tezacaftor

  • Theophylline

  • Tinidazole

  • Tipranavir

  • Tofacitinib

  • Tolterodine

  • Trabectedin

  • Trazodone

  • Dawa ya kuchoma ya triamcinolone acetonide

  • Triazolam

  • Vardenafil

  • Verapamil

  • Warfarin

  • Zanubrutinib

​

Metronidazole ikitumika na dawa zifuatazo inaweza kuleta madhara madogo;


  • Acetaminophen

  • Acetaminophen iv

  • Acetaminophen rectal

  • Alfentanil

  • Alfuzosin

  • Alosetron

  • Amitriptyline

  • Armodafinil

  • Atazanavir

  • Balsalazide

  • Biotin

  • Bosentan

  • Celecoxib

  • Cevimeline

  • Clarithromycin

  • Clomipramine

  • Dapsone

  • Desipramine

  • Diclofenac

  • Didanosine

  • Disopyramide

  • Docetaxel

  • Donepezil

  • Dutasteride

  • Efavirenz

  • Eplerenone

  • Estradiol vaginal

  • Ethanol

  • Eucalyptus

  • Finasteride

  • Flurbiprofen

  • Fluvastatin

  • Galantamine

  • Ibuprofen

  • Ibuprofen iv

  • Imatinib

  • Imipramine

  • Irinotecan

  • Irinotecan liposomal

  • Isradipine

  • Itraconazole

  • Ketoconazole

  • Lithium

  • Meloxicam

  • Montelukast

  • Nifedipine

  • Nimodipine

  • Nitrendipine

  • Nitroglycerin iv

  • Oxybutynin

  • Paclitaxel

  • Paclitaxel protein bound

  • Pantothenic acid

  • Parecoxib

  • Pimozide

  • Pioglitazone

  • Piroxicam

  • Propafenone

  • Pyridoxine

  • Pyridoxine (antidote)

  • Quinine

  • Ramelteon

  • Saxagliptin

  • Sufentanil

  • Sulfamethoxazole

  • Thiamine

  • Tolbutamide

  • Troleandomycin

  • Vesnarinone

  • Vinblastine

  • Vincristine

  • Vincristine liposomal

  • Vinorelbine

  • Voriconazole

  • Zaleplon

  • Ziprasidone

  • Zolpidem

  • Zonisamide

​

Maudhi madogo ya Metronidazole


  • Kupoteza hamu ya kula

  • Kupata Maambukizi ya kandida

  • Kuharisha

  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kichefuchefu

  • Kutapika

  • Ataksia

  • Kupata Mkojo uliopauka

  • Mwitikio wa disulfiram ikitumiwa pamoja na pombe

  • Mzio

  • Nutropenia

  • Ladha ya metaliki

  • Nuropathi

  • Pakreatitis

  • Degedege

  • Thromboflebaitis

  • Zerostomia

  • Ensefalopathi

  • Meninjaitis ya aseptiki

  • Nuropathi ya optik

  • Sindrome ya stevens Johnson

  • Necrosis ya Epidemo

  • Kupungua kwa hamu ya tendo la kujamiana

  • Maumivu wakati wa kukojoa

  • Proktaitiz

  • Maumivu ya maungio ya mwili

  • Saikosis

  • Kwikwi

  • Ugonjwa wa crohn’s

​

Marufuku ya metronidazole


Metronidazole ni marufuku kutumika kwa watu wafuatao;


  • Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa zilizo kwenye kundi la nitroimidazole

  • Mjamzito katika kipindi cha kwanza na cha pili

  • Mtu anayetumia disulfiram

  • Mgonjwa mwenye sindromu ya coockayne


Tahadhari


  • Degedege na homa ya uti wa mgongo ya aseptik huweza tokea endapo dawa itaongezwa dozi au kutumika kwa muda mrefu.

  • Kuna wagonjwa waliokwisha pata ensefalopathi na nuropathi ya pembeni

  • Ensefalopathi iliyolipotiwa ilikuwa inahusiana na dalili za ataksia, kizunguzungu na disiathria. Dalili hizi huisha wiki kadhaa tangu dawa imesimamishwa kutumika.

  • Nyuropathi ya pembeni ambayo huwa ni ya sensori huleta dalili za kufa ganzi au kuchomachoma kwa miguu

  • Kutumia dawa hii bila kuwa na ugonjwa uliothibitishwa kunaongeza kupata usugu wa vimelea vya bakteria na parasaiti mwilini mwako bila kuwa na faida yoyote kwako.

​

Mambo ya kufahamu kwa mtumiaji wa metronidazole

​

  • Matumizi ya muda mrefu yanaweza kukusababishia maambukizi makali

  • Tumia kwa umakini kwa mgonjwa mwenye figo iliyoferi, moyo kuferi, maambukizi ya H.Pyroli, na ini kuferi, wagonjwa wa agranulosaitosisi, leukopenia, na neutropenia

  • Acha kutumia pombe endapo unatumia dawa hii na kwa angalau siku tatu baada ya kuacha kutumia hii dawa.

  • Dawa hii inaweza kusababisha kukua kwa matiti kwa wanaume( gainekomastia)

  • Wagonjwa wenye maambukizi ya kandida, maambukizi hayo yanaweza kuongezeka Zaidi wakati wa matumizi ya dawah ii, hivyo ni vema mtu akatumia dawa za kutibu kandida

Metronidazole na ujauzito


  • Hakuna tafiti za kutosha za kuthibitisha madhara katika ujauzito. Tafiti zilizofanyika zinaonyesha kuwa matumizi ya dawa hizi wakati wa ujauzito haswa kipindi cha kwanza huongeza hatari ya kupata Watoto wenye mdomo sungura.

  • Dawa ya metronidazole huingia kwa mtoto kupitia kondo la nyuma, madhara kwenye uumbaji wa mtoto bado hayafahamiki. Tafiti zilizofanyika kwa panya pia hazionyeshi madhara kwa kichanga. Mtaalamu wa afya anatakiwa kuzingatia faida na harasa kwenye matumizi na kufikiria kuhusu madhara yanayoweza kujitokeza.

​

Metronidazole kipindi cha unyonyeshaji


Metronidazole huingia kwenye maziwa ya mama na hivyo mtoto anaweza kuipata kwa kunyonya maziwa na kiwango chake kwenye damu kikawa sawa na cha kwenye damu ya mama.


Kwa sababu ya madhara yake ya kusababisha uvimbe yaliyoonekana kwenye tafiti zilizofanyika kwa panya, mtaalamu wa afya unapotumia dawa hii kumbuka kuzingatia faida za matumizi kwa mama dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza kwa mtoto. Unaweza kuacha kutumia dawa hii kipindi cha dozi yote na masaa 24 toka kuacha kutumia dawa kabla ya kumruhsu mgonjwa kunyonyesha mtoto.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

16 Agosti 2023, 05:10:53

Rejea za mada hii:-

1. Metronidazole injection. https://www.pfizermedicalinformation.com/en-us/metronidazole/contradictions. Imechukuliwa 15.08.2023
bottom of page