Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Aprili 2020, 14:40:28
Natalizumab
Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa la monoklono antibodi, hufanya kazi kwa kuzuia chembe za damu za lyukosaiti kuingia kwenye mfumo wa fahamu wa kati na hivyo kupunguza inflamesheni na kuondolewa kwa mayelini za mishipa ya fahamu.
Natalizumab hupatikana kwenye mfumo wa maji na hutolewa kwa njia ya sindano inayochomwa kweney misuri.
Matumizi nachakula
Haina madhara yeyote inapotumika na chakula au pasipo na chakula.
Dozi ya dawa
Dozi yake hutumika kila baada ya siku 28
Uwezo wa dawa kupenya kwenye tishu
Dawa huwa na uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa fahamu wa kati.
Kazi za Natalizumab
Hutumika kutibu ugonjwa wa Matipo sklerosisi
Hutumika kutibu ugonjwa wa Crohn’s
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Natalizumab
Baricitinib
Beclomethasone, ya kunusa
Certolizumab pegol
Ifosfamide
Chanjo ya kirusi cha influenza
Lomustine
Mechlorethamine
Melphalan
Ocrelizumab
Procarbazine
Vedolizumab
Tahadhari ya Natalizumab
Huongeza hatari ya kupata ugonjwa endelevu wa Matifoko lyukoensephalopathi (PML)
Usitumie pamoja na dawa zingine za kushusha kinga ya mwili
Huweza kupelekea mzio
Huweza kupelekea kuvimba kwa ubongo
Huweza kupelekea kujeruhiwa kwa ini
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye mzio na dawa hii au mwenye historia ya kupata ugonjwa endelevu wa Matifoko lyukoensephalopathi (PML)
Matumizi ya Natalizumab kwa mama mjamzito
Hutumika kwa mama mjamzito pale tu faida zinapokuwa muhimu kuliko hasara.
Matumizi ya Natalizumab kwa anayenyonyesha
Kwa mama anayenyonyesha hapaswi kutumia sababu huweza kuleta athari kwa mtoto.
Maudhi ya Natalizumab
Kuchoka
Kuhara
Kukojoa mara kwa mara
Sinusaitiz
Maambukizi kwenye uke
Maumivu kwenye jointi
Kukohoa
Maambukizi ya virusi
Kuvimba ngozi
Maumivu ya koo
Kuvimba miguu
Kutokwa vipele
Maumivu kwenye hedhi
Masikio kupiga kelele
Kubeua gesi
Kuharibika kwa kazi za figo
Mzunguko wa hedhi kutokuwa katika mpangilio
Kujikojolea
Maumivu ya jino
Muwasho
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu
Kutokuona choo au choo kigumu
Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo
Tumbo kujaa gesi
Kutokuona hedhi
Je endapo umesahau dozi ya Natalizumab ufanyeje?
Endapo mgonjwa atasahau dozi anapaswa kuwasiliana na daktari aliyemuandikia dawa hii kwa maelekezo zaidi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Januari 2022, 19:15:23
Rejea za mada hii:-