Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Aprili 2020, 15:04:46
Olanzapine
Ni dawa ya kutibu magonjwa ya akili, iliyo kwenye kundi la antisaikotiki. Baadhi ya magonjwa hayo ni magonjwa ya schizophrenia na baipola.
Majina ya kibiashara
Olanzapine hufahamika kwa majina ya kibiashara kama;
Lybalvi
Olazax
Symbyax
Zalasta
Zypadhera
Zyprexa
Fomu ya Olanzapine
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge na maji yanayotolewa kwa kuchomwa sindano.
Olanzapine na chakula
Haina madhara yeyote ikitumika na chakula
Dawa kundi moja na olanzapine
Dawa zilizo kundi moja na Olanzapine
Quetiapine
Risperidone
Aripiprazole
Ziprasidone
Jinsi Olanzapine inavyofanya kazi
Dawa ya olanzapine hufunga milango ya kuingilia homoni za dopamine D1, D2, D4, histamine 5-HT2 na risepta za muskariniki.
Utoaji olanzapine mwilini
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya kinyesi na mkojo
Olanzapine hutibu nini?
Hutumika kutibu ugonjwa wa Schizofrenia
Hutumika kutibu magonjwa ya Baipola mania
Hutumika kutibu hali ya huzuni na sononeko(dipresheni)
Hutumika kuondoa hali ya kichefuchefu na kutapika inapotumika na Dexamethasone
Mwingilinao wa olanzapine na dawa zingine
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na olanzapine;
Apomorphine
Benzhydrocodone
Bomocriptine
Cabergoline
Dopamine
Entrectinib
Erdafitinib
Fedratinib
Fluvoxamine
Glasdegib
Hydrocodone
Hydroxychloroquine sulfate
Ivosidenib
Levodopa
Lisuride
Macimorelin
Mefloquine
Methyldopa
Ondansetron
Pefloxacin
Pitolisant
Pramipexole
Ropinirole
Safinamide
Siponimod
Sodium oxybate
Umeclidinium bromide
Vilanterol
Tahadhali ya olanzapine
Huweza kupelekea kupungua kwa kiasi cha chembechembe nyeupe za damu
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye daimenshia
Huweza kupelekea Kiharusi
Huweza kuathiri uwezo wa mtu kusimama wima kwa muda mrefu
Huweza kuathiri mtu kuwa hali ya kuchanganyikiwa
Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye aleji na dawa hii
Olanzapine na ujauzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama mjamzito
Olanzapine kipindi cha kunyonysha
Kwa mama anayenyonyesha haipaswi kutumika kwao sababu huingia kwenye maziwa.
Maudhi ya olanzapine
Hupelekea hali ya kuanguka baada ya mtu kusimama kwa muda mrefu
Kuongezeka uzito
Kuwa mdhaifu
Kizunguzungu
Kukosa usingizi
Kukosa Choo
Sukari kuwa juu
Shinikizo la damu kushusha
Kutetemeka
Kupunguza nguvu ya misuli
Je, kama umesahau dozi ya olanzapine ufanyeje?
Kama umesahau kutumia hii dozi yako ya olanzapine, tumia pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umeakaribia sana, subiri muda ufike ndipo utumie dozi hiyo kama alivyopangiwa na daktari.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:27:49
Rejea za mada hii:-