Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
Dawa za kutibu haja ngumu
13 Agosti 2023 09:17:53
Dawa nyongeza ya nyuzinyuzi.
Dawa hizi hufanya kazi kwa kuongeza ufyonzaji wa maji ndani ya utumbo na huvyo kutengeneza kinyesi chenye maji mengi. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha ili kuzuia utumbo kuziba kutokana na dawa hizi.
Baadhi ya dawa ni;
Calcium polycarbophil (FiberCon)
Methylcellulose fiber (Citrucel)
Psyllium (Konsyl, Metamucil)
Wheat dextrin (Benefiber)
Baadhi ya watu wanapata maudhi haya wanaotumia dawa hizi;
Tumbo kujaa gesi
Maumivu ya tumbo
Dawa za Osmotiki
Hufanya kazi ya kulainisha choo kwa kuongeza ufyonzaji wa maji kutoka mwilini kwenda kwenye utumbo mpana. Dawa hizo ni;
Magnesium citrate
Magnesium hydroxide
Lactitol
Polyethylene glycol
Baadhi ya maudhi ya dawa hizi ni;
Kuharisha
Kichefuchefu
Zitumike kwa umakini kwa wagonjwa wenye;
Magonjwa ya figo na moyo
Stimulant- Vichochea mjongeo misuli laini
Dawa hizi hufanya kazi kwa kuongeza kujongea kwa utumbo hivyo kusukuma kinyesi kitoke kwa haraka. Mtumiaji wa dawa hii atumie ana dalili kali na dawa zingine zilizoorodheshwa hapo juu hazijafanya kazi kama alivyotarajia. Baadhi ya dawa hizo ni;
Bisacodyl
Sennocides
Vilainisha haja kubwa
Hufanya kazi kwa kuongweeza majimaji kwenye kinyesi na kufanya choo kutoke kilaini. Dawa hizo ni Docusate sodium.
Dawa za kupachika
Dawa hizi huwekwa kwenye njia ya haja kubwa. Hufanya utumbo mpana uongeze mijongeo na hivyo kusukuma kinyesi. Dawa hizo ni Glycerin na Bisacodyl.
Enema
Dawa hii huwa mfumo wa maji na huingizwa kwenye njia
ya haja kubwa. Unawez akutumia maji ya bomba au dawa zingine kama bisacodyl au mafuta yenye madini kama enema ili kulainisha choo kigumu kwenye rektamu.
Dawa za kuandikiwa na daktari.
Dawa hizi lazima uandikiwe na daktari wako kabla ya kutumia. Dawa hizo hufanya kazi kwa kulainisha choo na hutumika kwa kunywa. Baadhi ya dawa hizo ni;
Lactulose
Linaclotide
Lubiprostone
Plecanatide
Polyethylene glycol
Prucalopride