​
Dalili na viashiria
Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
​
Dalili za DKA na viashiria mara nyingi hutokea kwa haraka sana, wakati mwingine ndani ya masaa 24. Kwa watu ambao hawajatambuliwa na tatizo la kisukari dalili na viashiria hivi huweza kumtia shuku kwamba mtu huyu anakisukari;
-
Kiu kupita kiasi
-
Kukojoa kupita kiasi
-
Kichefuchefu n kutapika
-
Maumivu ya tumbo
-
Uchovu na kuchoka mwili
-
Kuishiwa pumzi
-
Kutoa harufu nzuri kama ya matunda mdomoni
-
Kuchanganyikiwa
Dalili elekezi za DKA ambazo zniaweza kutambuliwa kwa kupima damu na mkojo huwa ni;
-
Kiwango cha juu cha sukari kwenye damu
-
Kiwango cha juu cha ketone kwenye mkojo
Wakati gani wa kumwona daktari
Kama unahisi unaumwa, una msongo wa mawazo, umeumwa mda uliopita au umejeruhiwa, pima sukari yako mara nyingi. Unaweza kujaribu kupima sukari kwa kutumia vipimo vinavyouzwa maduka ya madawa ili kuangalia asidi ya ketone.
Wasiliana na daktari wako haraka endapo;
Unatapika huwezi kula chakula ama kunywa
Kiwango cha sukari ni kikubwa kuliko kiwango cha kawaida na hakishuki kwa matibabu unayotumia nyumbani
Kiwango cha asidi ketone ni kikubwa kwa wastani ama kiwango cha juu
Tafuta msaada wa dharura endapo
-
Kiwango cha asidi ketone kimezidi miligramu 300 kwa desilita 1
-
Una asidi ya ketone kwenye mkojo na huwezi kuwasiliana na datary wako kwa ajili ya ushauri
-
Una dalili na viashiria vya DKA kama zilivyotajwa hapo juu
Kumbuka usipotibiwa hali hii ya DKA unaweza poteza maisha.
​
Imechapishwa 3/3/2015
Imeboreshwa 5/11/2018