top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Benjamin S, MD, Dkt. Adolf S, MD.

17 Aprili 2025, 06:46:27

Image-empty-state.png

Dalili za mimba ya miezi nane

Utangulizi

Mwezi wa nane wa ujauzito ni wakati muhimu katika kipindi cha mwisho cha ujauzito, ambapo mama na mtoto hupitia mabadiliko ya haraka ili kujiandaa kwa kujifungua. Katika kipindi hikimtoto hukua kwa kasi na mwili wa mama huanza kujiandaa kwa ajili ya leba. Huu ni wakati uliojaa furaha, matarajio, na dalili mbali mbali.


Je, ni zipi dalili za mimba ya miezi nane?

Katika hatua hii, mabadiliko ya homoni na ukuaji wa mtoto huleta dalili mbalimbali za kimwili na kihisia. Dalili za kawaida ni pamoja na:

  • Kupumua kwa shida: Mji wa mimba unavyokuwa huleta shinikizo katika diaframu (kiwambo0 hivyo kupumua huwa kugumu lakini haiathiri kiwango cha oksijeni mwilini.

  • Mwili kuchoka sana: Uzito wa ziada na kazi ya mwili kumlea mtoto hupelekea uchovu mkubwa.

  • Kwenda haja ndogo mara kwa mara: Mtoto anaposhuka chini kwenye fupanyonga, hugandamiza kibofu cha mkojo.

  • Kumvimba: Unaweza kuvimba miguu, vifundo vya miguu na mikono kutokana na      kuongezeka kwa maji mwilini

  • Mikazo ya uchungu wa uongo: Mikazo hii ya mazoezi ya leba inaweza kutokea mara kadhaa lakini haiambatani na maumivu

  • Maumivu ya mgongo: Uzito wa ziada na kuendelea kukua kwa tumbo huathiri mlingano wa mwili na kupelekea maumivu ya mgongo

  • Kukosa usingizi: Hii ni kutokana na hisia za wasiwasi, mkojo wa mara kwa mara, na usumbufu wa kimwili

  • Maziwa kuanza kutoka – Matiti huanza kutoa maziwa ya mwanzo (kolostrum) ambayo huwa na rangi ya njano


Mambo ya Kuzingatia

Kadri siku ya kujifungua inavyokaribia, kuna mambo muhimu ya kuzingatia:

  • Weka mpango wa kujifungua na uujadili na mtoa huduma ya afya

  • Andaa mfuko wa hospitali ukiwa na mahitaji yako na ya mtoto

  • Fuatilia miadi ya kliniki ya ujauzito

  • Hakikisha mtoto anacheza kila siku na toa taarifa kwa daktari kama kuna mabadiliko

  • Endelea kula mlo kamili na kunywa maji ya kutosha

  • Pumzika mara kwa mara na omba msaada kutoka kwa familia au marafiki.


Je, ni wakati gani unapaswa kumuona daktari?

Ingawa dalili nyingi ni za kawaida, baadhi ya hali zinahitaji uangalizi wa haraka wa kitabibu:

  • Mtoto kupunguza kucheza tumboni

  • Maumivu makali ya kichwa a kuona ukungu

  • Maumivu makali ya tumbo

  • Kutokwa damu au maji ukeni

  • Mikazo ya mara kwa mara yenye maumivu

  • Dalili za maambukizi  kama vile homa, kutetemeka, maumivu wakati wa kukojoa nk.


Wapi utapata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi nane?

Ili  kupata maelezo zaidi kuhusu mimba ya miezi nane bofya hapa.

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

17 Aprili 2025, 08:52:32

Rejea za dawa

  1. American College of Obstetricians and Gynecologists. (2020). Your pregnancy and childbirth: Month to month (6th ed.). ACOG.

  2. Mayo Clinic. (2025). Pregnancy week by week. https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/pregnancy-week-by-week/in-depth/pregnancy/art-20046767. Imechukuliwa 17.04.2025

  3. National Health Service (NHS). (2021). You and your baby at 32 weeks pregnant. https://www.nhs.uk/pregnancy/week-by-week/28-to-40-plus/32-weeks. Imechukuliwa 17.04.2025

  4. UpToDate. (2023). Prenatal care: Second and third trimesters. https://www.uptodate.com/contents/prenatal-care-second-and-third-trimesters. Imechukuliwa 17.04.2025

bottom of page