Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt Mangwella S, M.D
4 Desemba 2024, 16:05:21
Dalili za mimba ya mwezi mmoja
Utangulizi
Mimba ya mwezi mmoja ni sawa na ujauzito wa wiki nne. Dalili katika kipindi hiki husababishwa na muitikio wa mwili katika mabadiliko ya vichochezi vya ujauzito, dalili hizo hufanana na dalili zinazotokea kabla ya kuingia hedhi na hutofautiana kati ya mtu na mtu.
Je, ni zipi dalili za ujauzito wa mwezi mmoja?
Dalili kuu inayoonekana katika mimba ya mwezi mmoja ni kukosa hedhi na kuambata na miongoni mwa dalili zifuatazo;
Kichefuchefu
Kutapika
Hisia za gesi tumboni
Hisia ya kuvimbiwa
Matiti kujaa au kuuma
Kukojoa mara kwa mara
Uchovu mkali
Maumivu ya nyonga
Maumivu ya kubana na kuachia tumbo la chini
Joto la mwili kuongezeka
Mambo ya kuzingatia
Dalili nyingi za ujauzito wa mwezi mmoja hufanana na zile za kabla ya kuingia hedhi
Endapo unahisi dalili tajwa hapo juu na hujaingia hedhi fanya kipimo cha ujauzito kuwa na uhakika zaidi
Katika makala hii maneno ujauzito na mimba yametumuka kumaanisha kitu kimoja
Wapi utapata maelezo zaidi?
Ili kupata maelezo zaidi kuhusu ujauzito wa mwezi mmoja bofya hapa https://www.ulyclinic.com/umri-wa-mimba-kwa-miezi/mimba-ya-mwezi-mmoja. Unaweza pia kutazama video kuhusu mimba ya mwezi mmoja kwa kubofya hapa https://youtu.be/y-x6GXvAcQg?si=CFYUIUSkd0clg8sm
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
4 Desemba 2024, 17:59:54
Rejea za dawa
Common Pregnancy Complaints and Questions – Medscape Reference.https://emedicine.medscape.com/article/259724-overview#a1. Imechukuliwa 04.12.2024
Early Pregnancy Symptoms: 15 Signs and Timeline – Healthline. https://www.healthline.com/health/pregnancy/early-symptoms-timeline. Imechukuliwa 04.12.2024
Early pregnancy symptoms by days past ovulation (DPO) – MedicalNewsToday. https://www.medicalnewstoday.com/articles/322723. Imechukuliwa 04.12.2024