Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
3 Oktoba 2024, 05:04:01
Maji mengi kwenye chupa ya uzazi
Maji mengi kwenye ujauzito,ikifahamika pia kama maji mengi kwenye chupa ya uzazi hutambuliwa kwa kipimo kinachoitwa amniotiki fluidi Indeksi (AFI), kipimo hiki kinapozidi 24, mama husemekana ana maji mengi kwenye chupa ya uzazi.
Ā
Mambo muhimu ya kufahamu.
Ā
Mkojo wa mtoto ni chanzo kikuu cha uzalishaji wa maji kwenye chupa ya uzazi na mtoto anapokunywa majiĀ huwa chanzo kikuu cha kupunguza maji hayo
Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi husababishwa na matatizo ya figo au mirija ya mkojo wa mtoto kuziba au kutotengenezwa vema, kondo kutofanya kazi vema, chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati au mama kuishiwa maji-kukaukiwa
Sababu kuu za maji mengi kwenye chupa ya uzazi hazijulikani na ikifuatiwa na kusababishwa na ugonjwa wa kisukari kwa mama na mtoto maji
Matatizo ya mtoto yanayosababisha maji mengi kwenye chupa ya uzazi ni yale yanayoathiri uzalishaji, umezaji wa maji na matatizo ya kijusi haswa matatizo yaĀ mfumo wa tumboĀ au matatizo ya mfumo wa fahamu
ā
Matatizo gani husababisha maji mengi kwenye chupa ya uzazi?
Ā
Sababu zisizojulikana
Udhaifu katika uumbaji wa mtoto haswa mfumo wa tumbo na fahamu
Kisukari kwa mama (kisukari cha ujauzito)
Mapacha kuongezeana damu tumboni
Mtoto maji (fito haidrops)
Upungufu wa damu kwa kijusi
Kutooana kwa damu ya mama na mtoto
Maambukizi kwenye ujauzito
Ā
Karibia 2/3 ya sababu za maji mengi kwenye chupa ya uzazi huwa hazijulikani. Kuna ushahidi mwingine unasema kwamba maji mengi kwenye chupa ya uzaziĀ huambatana na matatizo kwenye vinasaba vya mtoto.
Ā
Ā
Dalili za maji mengi kwenye chupa ya uzazi
ā
Dalili zifuatazo huonekana kwa mama, dalili hizi hutokana na madhara ya maji hayo ndani ya tumbo la uzazi;
ā
Kuishiwa pumzi kwa mama
Kuvimba kwa tumbo na miguu
uchungu au kujisikia vibaya kwenye tumbo la chini
Mtoto kulala vibaya au kutanguliza matako
Tumbo la ujauzito kuwa kubwa
ā
Udhaifu gani wa uumbaji huhusiana na maji mengi kwenye chupa ya uzazi?
Ā
Maji mengi kwenye chupa ya uzazi huwa na mahusiano na madhaifu ya mfumo wa fahamu na tumbo. Tatizo kubwa la mfumo wa fahamu ni kama kuzaliwa ubongo wazi na magonjwa yanayohusiana na mishipa ya fahamu na misuli. Matatizo ya tumbo huwa ni kutofanyika kwa tundu endelevu kwenye mrija wa esofagasiĀ na au duodenum kutokana na madhaifu ya kiuumbaji. Pia tatizo la maji mengi huweza tokea kwenye ngiri katika kiwambo cha tumbo na kisababishi kingine ni matatizo ya valvu za moyo na matatizo ya mapigo ya moyo yasiyo ya mpangilio.
ā
Madhara ya maji mengi kwenye chupa ya uzazi
Ā
Maji mengi kwenye chupa ya uzazi huweza kusababisha;
ā
Kupasuka kwa chupa kabla ya wakati wake kwa sababu chupa hutanuka kuliko kawaida
Kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua kwa sababu kizazi hushindwa kusinyaa haraka.
Kujifungua mtoto njiti( kujifungua kabla ya wakati)
Kutangulia kwa kitovu cha mtoto wakati wa kujifungua- hii huwa hatari kwani mtoto anaweza kufa kutokana na kugandamizwa kwa mirija ya damu inayopeleka damu kwa mtoto
Kujifungua kwa oparesheni
Kunyofoka kwa kondo la nyuma
Mtoto kufia tumboni
Ā
Vipimo vya maji mengi kwenye chupa ya uzazi
ā
Kama umebainika kuwa na tatizo la maji mengi kwenye chupa ya uzazi, utafanyiwa kipimo cha picha mionzi sauti (ultrasound) ili kuangalia kiasi cha maji kwenye chupa ya uzazi. Kama wastani wa kiasi cha maji ya amniotiki kitakuwa sentimita 25 au zaidi, utasemekana kuwa na tatizo la maji mengi kwenye chupa ya uzazi.
ā
Wakati unafanyiwa kipimo hiki, mtaalamu wa kipimo hiki ataangalia pia kama mtoto ana madhaifu ya ki umbaji ya mtoto na madhara mengine
Ā
Unaweza kufanyia vipimo vingine pia kutokana na vihatarishi ulivyonavyo kwa uchunguzi wa mtoto na ujauzito wako kama vile;
ā
Kipimo cha damu ili kutambua magonjwa yanayosababishwa maji mengi kwenye chupa ya uzazi
Kipimo cha kuchukua maji kidogo kwenye chupa ya uzazi kwa ajili ya kipimo cha kromosome na karyotaipu
Ā
Pia utahitaji kufanyiwa vipimo vya mara kwa mara ili kuchunguza ujauzito wako kama vile;
ā
Kipimo cha mapigo ya moyo ya mtoto wakati anajongea
Kipimo cha maumbile yaĀ mtoto, kuangalia upumuaji wake, uchezaji wake na kiasi cha maji kwenye chupa ya uzazi
ā
Aina za maji mengi kwenye chupa ya uzazi
ā
Kuna aina tatu za maji mengi wkenye chupa ya uzazi ambazo zinatokana na majibu ya kipimo. Aina hizi husaidia kuamua aina ya matibabu.
ā
Maji mengi kiasi kidogo- Kipimo cha AFI kati ya 25- 30 cm
Maji mengi ya wastani- Kipimo cha AFI kati ya 30.1 hadi 35
Maji mengi kupita kiasi- Kipimo cha AFI zaidi ya 35.1
ā
Matibabu ya maji mengi kwenye chupa ya uzazi
ā
Kwa wanawake wenye maji mengi kiasi kidogo na maji mengi ya wastani, mara nyingi hawahitaji matibabu na tatizo linaweza kuisha lenyewe.
ā
Wanawake wenye magonjwa kama kisukari, endapo watapatiwa matibabu ya kisukari, tatizo hili la maji mengi huweza kupungua.
ā
Kama utapata dalili za uchungu kabla ya wakati au kuishiwa pumzi au maumivu ya tumbo kutokana na maji mengi kwenye chupa ya uzazi, unaweza kuhitaji matibabu ya kupunguziwa maji hayo kwa njia ya;
ā
Kupunguza maji yaliyozidi kwenye chupa ya uzazi kwa kutumia sindano maalumu
Kupewa dawa za kupunguza kiasi chamaji na uzalishaji wa mkojo wa mtoto unaochangia kuongezeka kwa maji ya chupa ya uzazi. Dawa inayotumika mara nyingi ni indomethacin. Dawa hii hairuhusiwi kutumika baada ya wiki 31 za ujauzito na huwa na hatari ya matatizo ya moyo kwa mtoto.
Ā
Baada ya matibabu hayo, uchunguzi wa kiasi cha maji kwenye chupa ya uzazi utafanyika kila baada ya wiki moja hadi mbili.
ā
Kama utakuwa na maji mengi kwa kiasi kidogo au wastaniĀ unaweza kuendelea na ujauzito mpaka utakapofikisha wiki 39 au 40 za ujauzito, kisha kujifungua.
ā
Kama utakuwa na kiasi kikubwa cha maji mengi kwenye chupa ya uzazi, utashauriwa na daktari ni wakati gani salama wa kujifungua bila madhara makubwa kwa mtoto.
ā
Ingawa tatizo hili linaleta hofu kubwa kwa mama, ni vema ukashirikiana na daktari wako ili kupata matibabu yatakayozuia madhara kwa kijusi na kwako.
ā
Kuna madhara ya kupunguza maji kwa sindano?
ā
Kuna hatari kidogo ya madhara ya kupunguza maji kwenye chupa ya uzazi yanayoweza kuwa;
ā
Kuanza kwa uchungu kabla ya wakati
Kunyofoka kwa kondo la nyuma
Kupasuka kwa chupa ya uzazi kabla ya wakati
Kujifungua njiti au kujifungua kabla ya wakati
Kufia kwa mtoto tumboni
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Oktoba 2024, 05:04:01
Rejea za dawa
Polyhydramnios. Merck Manual Professional Version. http://www.merckmanuals.com/professional/gynecology-and-obstetrics/abnormalities-of-pregnancy/polyhydramnios. Imechukuliwa 07.07.2020
Polyhydramnios. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 07.07.2020
Amniotic fluid disorders. In: Obstetrics: Normal and Problem Pregnancies. 7th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders ElsevierĶ¾ 2017. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 07.07.2020
National Health Service. Polyhydramnios (too much amniotic fluid). http://www.nhs.uk/conditions/polyhydramnios/Pages/polyhydramnios.aspx. Imechukuliwa 07.07.2020
Amniotic fluid index. https://en.wikipedia.org/wiki/Amniotic_fluid_index
Hamza, et al. Polyhydramnios: Causes, Diagnosis and Therapy. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3964358/#. Imechukuliwa 23.07.2021
Magann EF, et al. A review of idiopathic hydramnios and pregnancy outcomes. Obstet Gynecol Surv. 2007 Dec; 62(12):795-802.