top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Adolf S MD, na Dkt. Benjamin L MD

19 Februari 2024, 10:18:54

Image-empty-state.png

Vyakula wakati wa maandalizi ya kubeba ujauzito

Yapo  maandalizi mbalimbali ambayo wenza wanaokusudia kutafuta ujauzito wanapaswa kuyafanya. Miongoni mwa maandalizi hayo ni kuwa na lishe bora yenye virutubishi kutoka katika makundi yote ya vyakula.Mlo kamili husaidia kuuandaa mwili kuwa katika hali nzuri ya kutungisha na kuutunza ujauzito.

Umuhimu wa chakula katika mandalizi ya ujauzito

Zifuatazo ni faida za mlo kamili katika kipindi cha maandalizi ya kupata ujauzito kwa mwanamke na mwanaume;

  • Kupata virutubishi ambavyo husaidia mwili kufanya kazi vema na kuimarisha afya ya uzazi

  • Kusaidia kuongeza ubora wa mbegu za kiume na uovuleshaji

  • Kupunguza msongo katika mwili unaoweza kuathiri afya ya uzazi

  • Kuzuia mtoto kuzaliwa na kasoro za kimaumbile, mfano matumizi ya vyakula vyenye madini ya folate (foliki asidi)

  • Kuzuia upungufu wa damu katika kipindi cha ujauzito, mfano vyakula vyenye madini chuma

  • Kuufanya mwili uwe katika uzito unaoshauriwa kiafya, ambao una athari chanya katika afya ya uzazi

Vyakula unavyoshauriwa kutumia kwa wingi

Unashauriwa kutumia vyakula vifuatavyo kwa wingi unapokuwa katika maandalizi ya kutafuta ujauzito;

  • Vyakula vyenye madini ya zinki;

    Mfano wa vyakula hivi ni nyama, mimea jamii ya mikunde , nafaka zisizokobolewa, mbegu, karanga nk

  • Vyakula vyenye madini ya folate (foliki aside); Mfano wa vyakula hivi ni maini, mayai, mboga za majani za kijani nk

  • Vyakula vyenye vitamini hasa vitamin C; M

    fano wa vyakula hivi ni; atunda jamii ya limao, mboga za majani, mbegu nk

  • Vyakula vyenye madini chuma;

    Mfano wa vyakula hivi ni nyama, spinachi, maharagwe nk

  • Vyakula vyenye nyuzi nyuzi;

    Mfano wa vyakula hivi ni nafaka zisizokobolewa, mboga za majani, matunda nk

Vyakula ambavyo hupaswi kutumia

Matumizi  vyakula hivi kwa wingi huathiri afya ya uzazi:

  • Vyakula vya kusindika

  • Nafaka za kukobolewa

  • Vinywaji vyenye sukari nyingi

  • Vyakula vyenye mafuta mengi

  • Pombe

Wapi utapata maelezo zaidi

Kwa maelezo zaidi kuhusu maandalizi ya kufanya wakati wa kutafuta ujauzito bofya hapa https://www.ulyclinic.com/elimu-kwa-mjamzito-magonjwa/maandalizi-ya-kubeba-mimba

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Februari 2024, 10:41:50

Rejea za dawa

  1. Female Fertility and the Nutritional Approach: The Most Essential Aspects – NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC8634384/. Imechukuliwa 19.02.2024

  2. Diet and Nutritional Factors in Male (In) fertility—Underestimated Factors. NCBI. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7291266/. Imechukuliwa 19.02.2024

  3. 16 Natural Ways to Boost Fertility – Healthline. https://www.healthline.com/nutrition/16-fertility-tips-to-get-pregnant. Imechukuliwa 19.02.2024

  4. The Influence of Metabolic Factors and Diet on Fertility – PMC. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC10005661/. Imechukuliwa 19.02.2024

bottom of page