top of page

Mwandishi:

Dkt. Salome A, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

16 Aprili 2022 19:18:20

Image-empty-state.png

Wiki ya 13 ya ujauzito

Ni wiki inayoashiria kuisha kwa kipindi cha kwa cha ujauzi (mwezi wa kwanza mpaka watu) na mwanzo wa kipindi cha pili cha ujauzito (mwezi wa tano mpaka wa sita)


Nini hutokea kwa mtoto


  • Mtoto huendelea kuongezeka urefu na uzito, hata hivyo uzito huongezeka taratibu

  • Mifumo na viuongo mbali mbali huendelea kuimarika zaidi

  • Mtoto huendelea kucheza tumboni


Nini hutokea kwa mama


  • Uzalishwaji wa homoni za ujauzito hupungua na kupelekea dalili nyingi za ujauzito zinazomfanya mama kujisikia vibaya kuisha. Asilimia kubwa ya wajawazito hurejea katika hali ya kawaida na kufurahia maisha ya kila siku

  • Hamu ya kufanya ngono huongezeka japo si kwa wanawake wote

  • Mimba huanza kuonekana kwa nje

  • Kuanza kuongezeka uzito

  • Hatari ya kupata uti huongezeka


Nini cha kufanya


  • Kula mlo kamili na kufanya mazoezi kama inavyopendekezwa, na kuepuka matumizi ya pombe na sigara

  • Anza kuvaa nguo zenye nafasi zisizobana tumbo

  • Fanya kipimo cha ultrasound; itasaidia kubaini shida yoyote kwa mtoto na maendeleo kwa ujumla

  • Ongea na watoa huduma kliniki unapohisi dalili na viashiria vya U.T.I


Majina mengine


Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:

  • Ujauzito wa wiki 13

  • Mimba ya wiki 13

  • Wiki 13 ya mimba

  • Kijusi cha wiki 13

  • Mwonekano wa ujauzito wa wiki 13

ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa  ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

15 Julai 2022 18:50:28

Rejea za dawa

  1. Williams Obstetrics, 26e. CHAPTER 7: Embryogenesis and Fetal Developmenthttps://obgyn.mhmedical.com/content.aspx?bookid=2977&sectionid=250337469. 

bottom of page