Mwandishi:
Dkt. Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. MAngwella S, MD
30 Agosti 2022 18:03:11
Wiki ya 31 ya ujauzito
Kichwa cha moto huanza kuwa na mweonekano mzuri na nywele laini zilizofunika mwili huanza kupotea.
Nini hutokea kwa mtoto
Nywele laini ambazo zilikuwa zimefunika sehemu kubwa ya mwili wake katika wiki za awali huanza kupotea
Huanza kuwa na muonekano mzuri wa kichanga
Huwa mwenye nguvu zaidi na hivyo hucheza sana hali inayoweza kupelekea mama kukosa usingizi
Nini hutokea kwa mama
Mji wa uzazi hutanuka sana na kuanza kugandamiza diaframu hivyo kupelekea kushindwa kupumua vizuri, mgandamizo huu huwa na maudhi makali kuliko wiki za awali
Pia mgandamizo katika kibofu cha mkojo huongezeka na kusababisha kutokwa na mkojo bila hiari wakati wa kupiga chafya au kucheka kwa nguvu, pamoja na kukojoa mara kwa mara
Matiti huanza kutoa maziwa ya awali (dang’a) ambayo ni mazito yenye rangi ya njano, hata hivyo huweza kutokea mapema zaidi au karibia na wiki za kujifungua na wakati mwingine baada ya kujifungua
Nini cha kufanya
Fanya mazoezi ya kuimarisha sakafu ya nyonga (mazoezi ya kegeli) ili kuzuia hali ya kutokwa na mkojo bila hiari kuendelea baada ya ujauzito, japokuwa kwa asilimia kubwa ya wanawake hali hii huisha baada ya kujifungua (kusoma zaidi kuhusu mazoezi ya kegeli tembelea.
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 31
Mimba ya wiki 31
Wiki 31 ya mimba
Kijusi cha wiki 31
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 31
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 19:23:12
Rejea za dawa
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]