Mwandishi:
Dkt. Salome A, MD
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
1 Septemba 2022 18:16:19
Wiki ya 35 ya ujauzito
Mtoto huendela kuongezeka uzito na mwili wake kujiandaa kuishi nje ya tumbo la uzazi. Mama huendelea kuongezeka uzito na kuhisi dalili na maudhi mbali mbali.
Nini hutokea kwa mtoto
Mtoto huwa na urefu wa takribani sentimeta 43 na uzito wa gramu 2400
Mapafu huwa yamekomaa na endapo atazaliwa kipindi hiki basi hatakuwa na changamoto yoyote ya upumuaji
Kutokana na kuwa mkubwa na nafasi katika mji wa uzazi kuwa ndogo, mtoto hukunja miguu karibu kugusa kiwiliwili hivyo hukosa nafasi ya kujigeuza na kubaki na nafasi ya kuchezesha miguu na mikono tu.
Utando mweupe unaofunika ngozi yake huongezeka
Nini hutokea kwa mama
Kuanzia wiki hii na kuendelea mama huanza kuhisi kucheza kwa mtoto kunapungua tofauti na awali, badala yake huona na kihisi mtoto akirusha miguu au mikono kwa nguvu zaidi.
Hali ya maumivu yanayotokana na kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya kizazi huweza kuongezeka
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 35
Mimba ya wiki 35
Wiki 35 ya mimba
Kijusi cha wiki 35
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 35
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Septemba 2022 18:18:06
Rejea za dawa
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]