Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Episiotomi
Ni kuongeza njia uzazi kwa kukatwa kwa misuli ya uke na sehemu ya haja kubwa wakati mama anajifungua hasa mtoto aliye mkubwa kupita kawaida.
Wauguzi hufanya hivi endapo kuna dalili kuwa mtoto anayezaliwa hawezi kutoka kawaida bila njia kuongezwa au muda mwingine wanaochelewa kuongeza njia misuli ya kuta za uke huchanika yenyewe bila kukatwa hii ni kutokana na nguvu ya kusukuma mtoto
Ni wakati gani wa kuongezewa njia ya uzazi
-
Mtoto anapokuwa mkubwa na anahitaji nafasi kubwa zaidi ya kutoka
-
Bega la mtoto Linapokwama kwenye njia wakati wa kujifungua
-
Mapigo ya moyo yanapokuwa madogo au makubwa kupita kiasi wakati wa leba hii hulazimu kuongezewa njia mtoto atoke.
-
Leba kuwa kwa muda mrefu
-
Kama mama anahitaji msaada wakati kujifungua ,kuongezewa njia huweza kurahisisha hili zoezi
-
Kama mtoto ametanguliza matako
-
Kuzalishwa kwa mapacha
Mara nyingi wamama huongezewa njia kama tayari ashanza leba na kichwa kimetokeza tayari kwenye uke, hivyo huitaji kuongezewa njia haraka
Zipo sababu ambazo humtaka mama kujifungua kwa njia ya upasuaji
Lakini endapo mama huyu atafika hospitali tayari yupo kwenye hatua ya pili ya leba, huwalazimu manesi na wakunga kumzalisha na kukabiliana na changamoto ambazo wengine huishia kuongezewa njia lakini kama wangewahi hospitalini wangeweza kuandaliwa kwa ajili ya upasuaji
Hivyo mama pindi anaposikia dalili za labour anapaswa kuwahi hospitali mapema
Zifuatazo ni dalili ambazo hutokea kwa mama baada ya kuongezewa njia wakati wa kujifungua:
-
Maambukizi ya bakteria
-
Kuvimba
-
Damu kujikusanya (hematoma)
-
Damu kutoka kwa wingi
Baada siku chache kama mama atapata maambukizi ya bakteria wakati wa kuongezewa njia huweza kuona dalili zifuatazo;
-
Homa
-
Harufu mbaya ukeni
-
Kutokwa na usaha
-
Maumivu makali
Mara nyingi hutokea kama vifaa vilivyotumika vilikuwa ni vichafu
​
​
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ili dhidi ya afya yako.
​
Wasiliana na daktari wa ULY clinic kwa elimu na ushauri kupitia namba za simu au kubonyeza Pata Tiba chini ya tovuti hii.
​
​
Imeboreshwa mara ya mwisho 11.05.2020
​
Rejea
​
-
Health Line Labour and delivery. https://www.healthline.com/health/pregnancy/episiotomy-complications imechukuliwa 11/5/2020
-
EPISIOTOMY, John Hopskin https://www.hopkinsmedicine.org/health/treatment-tests-and-therapies/episiotomy?amp=true imechukuliwa 11/5/2020
-
Medline Plus , Episiotomy. https://medlineplus.gov/ency/patientinstructions/000483.htm imechukuliwa 11/5/2020
-
Episiotomy Medscape. https://emedicine.medscape.com/article/2047173-overview imechukuliwa 11/5/2020
​
​
​​
Bonyeza kusoma makala zingine zaidi kuhusu;
​
-
Huduma za kliniki wakati wa ujauzito
-
Namna ya Kujua tarehe ya kujifungua