Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjami L, MD
Alhamisi, 18 Novemba 2021
Beri nyeusi
Beri nyeusi ni matunda katika jamii ya matunda madogodogo jamii ya zabiabu, yanayopatikana kwa wingi huko kaskazini mwa Kanada na Marekani licha ya kuenea duniani kwa sasa.
Beri nyeusi zinasifika kwa umahiri wake pale linapokuja suala afya kwani zimekua zikitumika kwa matibabu kupitia tibalishe, hii ni kutokana na uwezo na wingi wa virutubisho muhimu kwa mwili wa binadamu. Unaeza tumia beri nyeusi kama sharubati, mvinyo , kuoka pia kulitumia kama lilivyo.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye berinyeusi
Kabohaidreti
Protini
Nyuzilishe
Mafuta
Sukari
Vitamini
Madini
Viinilishe vinavyopatikana kwenye berinyeusi yenye gramu 100
Nishati = 43kcal
Mafuta = 0.49g
Sukari = 4.88g
Nyuzilishe = 5.3g
Kabohaidreti = 9.16g
Protini = 1.39g
Vitamini zinazopatikana kwenye berinyeusi yenye gramu 100
Vitamini A = 214IU
Vitamini B1 = 0.020mg
Vitamini B2 = 0.026mg
Vitamini B3 = 0.646mg
Vitamini B6 = 0.030mg
Vitamini B9 = 25mcg
Vitamini C = 21mg
Vitamini E = 1.17mg
Vitamini K = 19.8mcg
Madini yanayopatikana kwenye berinyeusi yenye gramu 100
Potashiamu = 162mg
Magineziamu = 20mg
Fosifolasi = 22mg
Sodiamu = 1mg
Madini chuma = 0.62mg
Kalishiamu = 29mg
Zinki = 0.53mg
Faida za kiafya zitokanazo na matumizi ya berinyeusi
Hutengeneza na kuimarisha mifupa
Huimarisha misuli na mishipa ya damu
Hupunguza athari zitokanazo na baridi yabisi
Huimarisha afya ya ngozi
Husaidia na kuimarisha mmeng`enyo wa chakula
Huimarisha kinga ya mwili
Hutibu na kuzuia matatizo ya kinywa
Imeboreshwa,
18 Novemba 2021, 10:40:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Watts, d.c. (2007). Dictionary of plant lore (rev. Ed.). Oxford: academic. P. 36. Isbn 978-0-12-374086-1.
Folta, , et al (2011). Genetics, genomics and breeding of berries. Crc press. Pp. 69–71. Isbn 978-1578087075.
Marrone, et al(2011). Indiana, kentucky, and ohio wild berries & fruits. Teresa marrone. P. 272.