Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Chungwa
Chungwa ni tunda lenye viinirishi na vitamin zaidi ya 20 ikiwemo vitamin C, nyuzinyuzi vyenye umuhimu mkubwa katika mwili. Ulaji wa chungwa hukinga mwili dhidi ya magonjwa ya kisukari, moyo, mifupa na ngozi na nywele na pumu n.k.
Unaweza kutumia chungwa kwa kufyonzwa maji yake, kutengeneza sharubati, na pia unaweza kula chungwa pamoja na nyuzinyuzi zake. Maganda ya chungwa pia huweza tumika kutengeneza chai yenye virutubisho vingi.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye chungwa
Protini
Nyuzilishe
Mafuta
Madini
vitamini
Sukari
Maji
Viinilishe vinavyopatikana kwenye chungwa lenye gramu 100
Nishati = 63KJ
Kabohaidreti = 16g
Mafuta = 0.3g
Nyuzilishe = 4.5g
Sukari = 11g
Maji = 82.3g
Madini yanayopatikana kwenye chungwa lenye gramu 100
Kalisiamu = 70mg
Kopa = 0.050mg
Chuma = 0.80mg
Magnezium = 14mg
Fosifolasi = 22mg
Potassium = 196mg
Sodiumu = 2mg
Zinki = 0.11mg
Vitamini zinazopatikana kwenye chungwa lenye gramu 100
Vitamini a = 13mg
Vitamini B1 = 0.1mg
Vitamini B2 = 0.05mg
Vitamini B3 = 0.5mg
Vitamini B5 = 0.33mg
Vitamini B6 = 0.093mg
Viatmini B9 = 30mcg
Vitamini C = 71mg
Faida za kiafya za ulaji wa machungwa
Huongeza hamu ya kula
Huimarisha kinga ya mwili hivyo kuukinga dhisi ya magonjwa
Huzuia mwili kupoteza maji
Huimarisha afya ya ngozi na mifupa
Imeboreshwa,
9 Mei 2022, 14:55:03
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Franke, Adrian A et al. “Bioavailability and antioxidant effects of orange juice components in humans.” Journal of agricultural and food chemistry vol. 53,13 (2005): 5170-8. doi:10.1021/jf050054y.
United states standards for grades of florida oranges and tangelos (usda; february, 1997)
Citrus direct". Freshcitrusdirect.wordpress.com. Archived from the original on 2015-01-10.
Perez-cacho pr, rouseff rl (2008). "fresh squeezed orange juice odor: a review". Crit rev food sci nutr. 48 (7): 681–95.