Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sima A, CO
Dkt. Charles W, MD
Ijumaa, 10 Aprili 2020

Faida za Alizeti mwilini
Mmea wa alizeti hutoa mbezu za alizeti zinazotumika kutengeneza mafuta mazuri yasiyo na kihatarishi kikubwa cha kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Mbegu ya alizeti huwa na vitamini E, madini ya kopa, manganezi, seleniamu kwa wingi na mafuta ya omega 3 kwa wastani pamoja na virutubisho vingine ambavyo ni;
Vitamin A, C, D,K, B1, B2,B3, B5, B6, B12,
Madini ya Folate, cholini, Fosforasi,
Madini ya kolini
Wanga
Viinilishe vinavyopatikana kwenye mbegu za alizeti
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Sukari
Maji
Mafuta
Protini
Vitamini
Maji
Viinilishe vinavyopatikana kwenye mbegu za alizeti zenye gramu 100
Nishati = 584kcal
Protini = 20.78g
Sukari = 2.62g
Mafuta = 51.46g
Nyuzilishe = 8.6g
Kabohaidreti = 20g
Maji = 4.7g
Vitamini zinazopatikana kwenye mabegu za alizeti zenye gramu 100
Vitamini B1 = 1.48mg
Vitamini B2 = 0.355mg
Vitamini B3 = 8.335mg
Vitamini B5 = 1.13mg
Vitamini B6 = 1.345mg
Vitamini B9 =227mcg
Vitamini C = 1.4mg
Vitamini E = 35.17mg
Madini yanayopatikana kwenye mbegu za alizeti zenye gramu 100
Kalishiamu = 78mg
Potashiamu = 645mg
Madini chuma = 5.25mg
Magineziamu = 325mg
Manganaizi = 1.95mg
Sodiamu = 9mg
Zinki = 5mg
Fosifolasi = 660mg
Faida za alizeti
Alizeti huwa na faida zifuatazo;
Huchochea afya nzuri ya moyo kutokana na mafuta yake kutokuwa na kolestro mbaya ya LDL
Hupelekea afya nzuri ya ngozi kutokana na kuwa na wingi wa Vitamin A na E
Huchochea mwili kuwa na nguvu kutokana na kuw ana wanga
Huweza kuimarisha nywele na kuzifanya zisikatike katike kutokana na kuwa na vitamini E
Huimarisha kinga ya mwili kutokana na kuw na madini ya selenium na vitamini
Husaidia mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kwenda kwa haraka
Husaidia kupunguza kolestro ya LDL mwilini
Husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani kutokana na kuwa na kuwa na antioksidanti kwa wingi
Hupunguza inflamesheni mwilini, hivyo huwa na faida kwa wagonjwa watu wenye pumu
Husaidia kupunguza chunusi kwa kuwa na wingi wa Vitamin A na E
Husaidia kupunguza hali ya kuzeeka mapema kutokana na wingi wa antioksidanti
Hupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu la juu
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 16:59:48
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Global Health Benefits of sunflower. https://globalhealing.com/natural-health/health-benefits-of-sunflower-seeds/amp/. Imechukuliwa 10/4/2020
Good food for good. Sunflower Oil. https://goodfoodforgood.ca/2019/06/06/good-food-for-good-amazing-benefits-of-sunflower-seeds/. Imechukuliwa 10/4/2020
EATING WELL SUNFLOWER OIL. http://www.eatingwell.com/article/2059940/sunflower-seeds-nutrition/. Imechukuliwa 10/4/2020
Health Line Sunflower oil. https://www.healthline.com/nutrition/sunflower-seeds. Imechukuliwa 10/4/2020
Seeds, sunflower seed kernels, dried. https://nutritiondata.self.com/facts/nut-and-seed-products/3076/2. Imechukuliwa 10/4/2020
Manwaring, W H. “Nutritional Value of Sunflower Seed.” California and western medicine vol. 63,3 (1945): 112.
Ciarka D, et al. (2009). "Allelopathic potential of sunflower. I. Effects of genotypes, organs and biomass partitioning". Allelopathy Journal. 23 (1): 95–109.
Marzinek, et al. (September 2008). "Cypsela or achene? Refining terminology by considering anatomical and historical factors". Revista Brasileira de Botânica. 31 (3): 549–553.
Leather GR (1987). "Weed control using allelopathic sunflowers and herbicide". Plant and Soil. 98: 17–23.