top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sima A, CO

Dkt. Adolf S, MD

Jumapili, 19 Aprili 2020

Faida za Vitamin A
Faida za Vitamin A

Vitamini A ni miongoni mwa virutubisho vilivyo katika kundi la virutubibsho vinavyo hitajika kwa kiasi kidogo lakini vyenye kazi muhimu sana mwilini.


Vitamini A ina kazi muhimu mwilini na kabla ya kuziangalia ebu tujue aina na vyanzo vya vitamini A.


Vyanzo vya vitamini A


  • Nyama

  • Maini

  • Samaki

  • kiini cha yai

  • maziwa ya mama anaenyonyesha

  • Siagi ya maziwa

  • Mboga na matunda yenye rangi ya njano mfano nyanya, karoti, maembe, papai, tikiti maji, zabibu, viazi vya njano na mahindi ya njano


Umuhimu na kazi za vitamini A


Nimuhimu kwa afya ya macho kwani vitamini A huunda sehemu muhimu ya seli za macho ili kuona vizuri. Ukosefu ama upungufu wa vitamini A hupelekea uono hafifu wa macho hususani kwenye giza ama kwenye mwanga hafifu.


  • Huimarisha kinga ya mwili ili kupambana dhidi ya magonjwa na mambukizi mbalimbali

  • Huimarisha afya ya mfumo wa uzazi na uumbaji wa mtoto wakati wa ujauzito

  • Husaidia ukuaji hususani kwa watoto

  • Husaidia ukuaji na uimara wa meno na mifupa

  • Husaidia kupambana na sumu mbalimbali mwilini

  • Husaidia mwili katika kutengeneza damu.

  • Hupunguza hatari ya kupata saratani kama vile saratani ya mapafu, kibofu, mlango wa kizazi(seviksi)


Mahitaji ya vitamin A kwa siku


Makundi tofauti tofauti kama vile watoto, vijana wanao balehe, mama mjamzito au anayenyonyesha, wanaume na wanawake wana mahitaji ya viwango vinavyotofautiana kwa siku.


Athari za upungufu wa vitamini A


  • Kushindwa kuona vizuri kwenye giza au mwanga hafifu.

  • Kupata ngozi kukauka na kupauka na kua na vidonda pamoja na nywele zisizo na afya.

  • Kupata maambukizi ya magonjwa mara kwa mara haswa katika mfumo ya njia ya hewa, Gastrointestino na mfumo wa mkojo

  • Watoto kuugua surau kwa urahisi

  • Kudumaa kwa watoto kutonana na kukoma kukua na kuongezeka uzito

  • Ukuaji wa taratibu na wenye kasoro wa mifupa na meno


Athari za kuzidi kwa vitamini A


Licha ya kua vitamini A ni muhimu mwilini, virutubisho hivi vina madhara fulani endapo vitazidi mwilini. Ni muhimu kukumbuka kua athari hizi huonekana zaidi kwenye matumizi ya dawa zenye virutubisho vya vitamini A


Athari hizo ni pamoja na


  • Kuhisi kizunguzungu

  • Kuhisi kichefuchefu

  • Kuhisi maumivu ya kichwa

  • Mzio

  • Maumivu ya viungo na mifupa

  • Kupoteza fahamu

  • Mtoto aliye tumboni kuumbika kimakosa kama mama mjamzito akizidasha matumizi ya dawa zenye vitamini A

  • Kunyonyoka nywele

  • Udhaifu wa mifupa na inakua rahisi kuvunjika

  • Ukosefua wa usingizi


Ni muhimu kukumbuka kwamba athari hizi huisha kwa kusitiasha matumizi ya virutubisho dawa za vitamini A au kula kiwango sahihi cha vitamini A.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:13:17
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. NIH. Vitamin A Fact Sheet for Consumers. https://ods.od.nih.gov/pdf/factsheets/VitaminA-Consumer.pdf. Imechukuliwa 18.04.2020

  2. Healthline. 6 Health Benefits of Vitamin A, Backed by Science.https://www.healthline.com/nutrition/vitamin-a-benefits#section8. Imechukuliwa 18.04.2020

  3. Vitamin A. Office of Dietary Supplements, National Institutes of Health. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminA-HealthProfessional/. Imechukuliwa 18.04.2020

  4. Vitamin A oral. Facts & Comparisons eAnswers. http://www.wolterskluwercdi.com/facts-comparisons-online/. Imechukuliwa 18.04.2020

  5. Bexarotene. Micromedex 2.0 Healthcare Series. http://www.micromedexsolutions.com. Imechukuliwa 18.04.2020

  6. Vitamin A. Natural Medicines. http://www.naturalmedicines.therapeuticresearch.com. Imechukuliwa 18.04.2020

bottom of page