Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Alhamisi, 16 Aprili 2020
Faida za madini ya Zinki mwilini
Ni madini yanayofanya kazi nyingi mwilini, madini haya hayatengenezwi mwilini, ila yanapatikana kwenye vyakula. Unapaswa kula vyakula vyenye madini haya kwa wingi ili kuzuia upungufu wake na madhara yanayoweza kujitokeza.
Umuhimu wa zinki
Zinki huhitajika mwilini kwa ajili ya;
Shughuli za vimeng’enya
Kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
Utengenezwaji wa protini
Utengenezwaji wa DNA
Kuponya vidonda
Ukuaji na maendeleo ya mwili
Kuzuia kuharisha kwa kuponya mfumo wa Gastrointestino
Madini haya hupatikana wa wingi kwenye mimea na vyakula vya Wanyama
Kazi za zinki mwilini
Husaidia kuchochea vimeng’enya zaidi ya 300 ambao hutumika katika umeng’enyaji wa chakula
Huimarisha mfumo wa kinga za mwili na kusaidia mwili upambane na maradhi.
Hutumika katika uzalishaji wa protini muhimu mwilini na utengenezwaji wa DNA
Huongeza kasi ya uponyaji wa vidonda
Hutumika kuondoa chunusi, watu wengi ambao hupata chunusi ni wale ambao wana madini ya zinc kwa uchache ,hivyo kutumia vyakula vyenye madini ya zinki au dawa mbadala huweza kutoa chunusi
Hupunguza inflamesheni kwenye seli
Dalili za upungufu wa zinki
Huathiri mfumo wa kinga ya mwili
Huathiri ukuaji na maendeleo ya mwili
Huchelewesha ukuaji kijinsia
Kutokwa na vipele kwenye ngozi
Kuhara
Vidonda kutokupona mapema
Vyanzo vya madini zinki
Samaki jamii ya shellfish
Nyama
Nyama za Wanyama jamii ya ndege
Mboga jamii ya kunde
Mayai
Mbegu zisizokobolewa
Baadhi ya mboga za majani kama bamiia,uyoga na kunde
Zipo dawa za mbadala za kutumia kwa mtu mwenye upungufu wa madini ya zinki
Dawa hizi hutolewa katika mfumo wa tembe, vidonge na maji
Dawa hizi zinapotolewa kwa wingi huweza kupelekea madhara kama;
Kichefuchefu
Kutapika
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kubana kwa tumbo
Kupua kwa kinga ya mwili
Ili kuepuka dozi kubwa unapaswa kutumia kwa dozi jinsi ambavyo utakuwa umeelekezwa na daktari
Mama mjamzito na anayenyonyesha mahitaji ya madini haya huongezeka kufikia miligramu 11 hadi 12 kwa siku
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:13:42
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
WebMd.Zinc.https://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-982/zinc. Imechukuliwa 14/4/2020
MedicalNewTodau.zinc.https://www.medicalnewstoday.com/articles/263176. Imechukuliwa 14/4/2020
HealthLine.ZincMineral.https://www.healthline.com/nutrition/zinc. Imechukuliwa 14/4/2020
Mayoclinic.Zinc.https://www.mayoclinic.org/drugs-supplements-zinc/art-20366112. Imechukuliwa 14/4/2020