top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Sospeter B, MD

Jumamosi, 4 Desemba 2021

Kiazisukari
Kiazisukari

Kiazisukari ikifahamika pia kama biti au beet ni zao la mzizi, huwa na umbo la duara na hushamiri kwa majimaji yenye rangi na hivyo kuifanya kuwa na mwonekano wa rangi nyekundu. Mmea wa kiazi sukari pia huwa na rangi inayofanana na kiazi.


Asili ya kiazi sukari


Asili ya zao hili ni huko Kanada na Marekani na ndiko linakolimwa kwa wingi na kusambazwa duniani kote.Kama ilivyo kwa mazao mengine ya mizizi, kiazisuakari pia hupendwa kuliwa kutokana na uwepo wa virutubisho na madini ya kutosha kwa ajili matumizi na afya ya binadamu. Unaweza kutumia kiazi hiki kwa kula kama kilivyo, kupika/kuchemshwa au kutengeneza sharubati.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye kiazisukari


  • Mafuta

  • Nyuzilishe

  • Sukari

  • Madini

  • Vitamini

  • Maji

  • Kabohaidreti

  • Protini


Viinilishe vinavyopatikana kwenye kiazisukari chenye gramu 100


  • Nishati = 43kcal

  • Protini =1.6g

  • Nyuzilishe =2.8g

  • Mafuta= 0.2g

  • Maji =87.6g

  • Sukari = 6.8g

  • Kabohaidreti = 9.6g


Vitamini zinazopatikana kwenye kiazisukari chenye gramu 100


  • Vitamini A =2mcg

  • Karotini Beta = 20mcg

  • Vitamini B1 =0.031mg

  • Vitamini B2 =0.040mg

  • Vitamini B3 = 0.334mg

  • Vitamini B5 =0.155mg

  • Vitamini B6 = 0.067mg

  • Vitamini B9 = 109mcg

  • Vitamini C = 4.9mg

  • Vitamini E =0.04mg

  • Vitamini K = 0.2mcg


Faida za kiazisukari


Unaweza kupata faida zifuatazo kwa kula kiazi sukari;


  • Kurekebisha shinikizo la damu

  • Kuimarisha mjongea wa viungo(wanamichezo wanashauriwa kula kiazisukari masaa 2 mpaka 3 kabla ya michezo kwa matokeo bora)

  • Kuongeza kinga ya mwili

  • Kuimarisha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula

  • Kuimarisha afya ya Ubongo pamoja na moyo

  • Kusaidia kkupunguza kasi ya uginjwa wa kusahasahau

  • Kupunguza kasi ya kupatwa/kushambuliwa na kansa za aina mbalimbali

  • Kusaidia kupunguza uzito usiotakiwa mwilini

Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 16:07:35
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Joris P.J, et al. Beetroot juice improves in overweight and slightly obese men postprandial endothelial function after consumption of a mixed meal. Atherosclerosis. 2013;231:78–83.

  2. Winkler C, et al. In vitro effects of beet root juice on stimulated and unstimulated peripheral blood mononuclear Cells. Am. J. Biochem. Biotechnol. 2005;1:180.

  3. Frank T, et al. Urinary pharmacokinetics of betalains following consumption of red beet juice in healthy humans. Pharmacol. Res. 2005;52:290–297.

  4. Pietrzkowski Z, et al. Influence of betalin-rich extracts on reduction of discomfort associated with osteoarthritis. New. Med. 2010;1:12–17.

  5. Ormsbee M.J, et al. Beetroot juice and exercise performance. J. Int. Soc. Sports Nutr. 2013;5:27–35.

  6. Clifford, Tom et al. “The potential benefits of red beetroot supplementation in health and disease.” Nutrients vol. 7,4 2801-22. 14 Apr. 2015, doi:10.3390/nu7042801

bottom of page