Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Jumatano, 3 Novemba 2021

Kitunguu maji
Kitunguu maji ni zao linalopatikana kwenye kundi la mbogamboga, zao hili kimekua maarufu kwa matumizi ya kiungo kwenye chakula. Huweza kuliwa kikiwa bichi, kukaangwa au kuchemshwa,Hutegemea na mtumiaji.Zao hili ni salama kabisa kiafya na wataalamu wamekua wakishauri litumike ili kuboresha afya ya mlaji.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye kitunguu maji
Mafuta
Sodium
Potashiamu
Kabohaidreti
Protini
Madini Chuma
Vitamini
Magineziamu
Nyuzilishe
Sukari
Zinki
Viinilishe vinavyopatikana kwa kutumia kitunguu maji gramu 100
Sodiamu - 2gm
Mafuta - 0.2gm
Kabohaidreti - 20gm
Nyuzilishe - 4.3gm
Protini - 1gm
Maji - 174.5gm
Sukari - 4.2gm
Madini yanayopatikana kwenye kitunguu maji kwa mlo wa gramu 100
Vitamini C -
Kalishiamu - 33.4gm
Kopa - 0.114mg
Madini Chuma - 0.47mg
Magineziamu - 22.46mg
Potashiamu - 388mg
Zinki - 0.33mg
Kemikali za kitunguu
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye kitunguu maji
Kemikali itwaayo Allium
Zifuatazo ni faida za vitunguu maji katika mwili wa binadamu
Kuimarisha afya ya ngozi na Nywele
Kurekebisha shiniko la Damu
Kuimarisha kinga ya mwili
Kupunguza hatari ya kupata saratani za aina mbalimbali
Kuupa mwili hamasa (kuchangamsha mwili)
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:02:41
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Clifford A. Wright. Mediterranean Vegetables: A Cook's ABC of Vegetables and their Preparation in Spain, France, Italy, Greece, Turkey, the Middle East, and North Africa, with More than 200 Authentic Recipes for the Home Cook. (Boston: Harvard Common Press, 2001). pp. 300-301
Rolland, Jacques L. Sherman, Carol (2006). The Food Encyclopedia. Toronto: Robert Rose. pp. 335–338. ISBN 9780778801504.
Atlanta, GA: Agency for Toxic Substances and Disease Registry, US Department of Health and Human Services. October 2012.
Williams, Sue Rodwell; Long, Sara (1997). Nutrition and diet therapy. p. 229. ISBN 978-0-8151-9273-2.