Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Adolf S, MD
Jumapili, 12 Aprili 2020
Kolestrol kwenye damu
Kolestro ni neno tiba linalotumika hapa ULY clinic, limetokana na neno tiba “cholesterol” ambalo asili yake ni kigiriki likiwa linamaana ya kampaundi ngumu ya sterol inayopatikana kwenye tishu za Wanyama wote, damu, nyongo, na mafuta ya Wanyama. Kwa Kiswahili jina ambalo linafahamika ni lehemu.
Mwili unahitaji kolestro ili uweze kutengeneza homoni , vitamin D na vimeng’enya vya chakula. Kolestro nyingi kupita kiasi kwenye mishipa ya damu huweza kutengeneza plagi kwenye mishipa hiyo na kufanya ipungue kipenyo -atherosklerosisi, au kuziba kabisa. Kuziba kwa mishipa ya damu huweza kusababisha magonjwa mbalimbali kama mshituko wa moyo na kiharusi.
Upo muunganiko wa mafuta na protini ambao huweza kutengeneza kolestro tofauti kwenye mwili kama ifuatavyo;
Lipoprotini yenye ujazo mkubwa-HDL
Lipo protini yenye ujazo mdogo-LDL
Lipoprotini yenye ujazo mdogo Zaidi-VLDL lipoprotein
Lipoprotini yenye ujazo mkubwa-HDL
Hukulikana kama kolestro nzuri kwa sababu hubeba kolestro mbaya kutoka sehemu zingine za mwili na kupeleka kwenye Ini , ini hufanya kazi ya kuondoa kolestro mwilini.
Lipo protini yenye ujazo mdogo-LDL
Hii hujulikana kama kolestro mbaya kwa sababu hii hutengeneza plagi ndani ya mishipa ya dam una kuifanya kuwana kipenyo kidogo au kuziba kabisa.
Lipoprotini yenye ujazo mdogo Zaidi-VLDL lipoprotein
Hii pia ni kolestro ambayo ni mbaya zaidi sababu hupelekea kutengenezwa kwa plagi kwenye mishipa ya damu na kuifanya kuwa miembamba, pia hubeba mafuta ya traiglaiseraids kwa wingi.
Mambo yanayoongeza kolestro kwenye damu
Tabia ya kutokula kiafya:- kula kwa wingi vyakula vyenye mafuta kwa wingi kama nyama za kukaanga au zenye Mafuta, chokoleti, vyakula vya kukaanga, vyakula vya viwandani.
Kutofanya mazoezi na kukaa kwa muda mrefu:- Kutokufanya mazoezi huongeza kiasi cha kolestro mwilini. Kufanya mazoezi huongeza mwili kutumia Mafuta mwilini.
Kuvuta sigara:- Hii hali huweza kuongeza kolesto kwa kupunguza kiasi cha lipoprotini yenye ujazo mkubwa
Makundi yaliyo hatarini kuwa na kolestro nyingi
Umri mkubwa zaidi; Kadri umri unavyozidi kuwa mkubwa zaidi kolestro katika mwili huzidi kuwa kubwa ,kwa watoto wadogo na vijana ni wachache sana huweza kuwa na kolestro kubwa
Kurithi; Hali ya kolestro kuwa juu inaweza kuwa ni hali ya kifamilia ambayo hurithisha kwa watoto wa Familia
Kuwa na uzito kupita kiasi; Kuwa na uzito kupita kiasi huweza kuongeza kiasi cha kolestro mwilini
Kabila: Jamii ya waafrika wengi huwa na kolestro kwa wingi kupita wazungu
Vyakula vyenye kolestro nyingi
Mayai: Yai moja huweza kuwa na kolestro Milligram 211
Nyama za ogani kama moyo, maini,
Vyakula vya kukanga
Nyama za kusindikwa viwandani
Vyakula vinavyoandaliwa kwa sukari na mafuta mengi kama keki ,sukari ya barafu
Samaki wenye magamba kama shrimp na crab
Maziwa mgando
Jibini
Vyakula vyenye kolestro kidogo
Kunde, maharage, mbaazi
Parachichi
Samaki mfano aina ya salmon
Matunda kwa wingi
Maharage ya soya
Mboga za majani
Majani ya mboga za kijani
Njia nzuri za kiafya kuepuka kolestro kwenye damu
Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kama matunda, maharage, kunde
Kufanya mazoezi kwa kwa ratiba maalumu
Kupunguza uzito
Kuacha tabia zisizo za kiafya kama kula vyakula vya mafuta sana
Kula matunda kwa wingi
Magonjwa yatokanayo na kolestro nyingi
Shinikizo la juu la damu
Kisukari
Kuferi kwa moyo
Kiharusi
Vipimo kwa ajili ya kolestro mwilini
Kipimo cha kupima jumla ya kolestro mwilini:- kipimo hiki huweza kupima aina zote za kolestro mwilini
Kipimo cha kolestro wakati wa mfungo wa usiku:- Hiki huweza kuonyesha kolestro na triglycerides
Dawa zinazoshusha kiasi cha lehemu mwilini
Atorvastatin (Lipitor)
Fluvastatin (Lescol)
Lovastatin
Pitavastatin (Livalo)
Pravastatin (Pravachol)
Rosuvastatin calcium (Crestor)
Simvastatin (Zocor)
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:15:10
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Cholesterol. https://www.dictionary.com/browse/cholesterol. Imechukuliwa. Imechukuliwa 12/4/2020
Health Line Cholesterol https://www.healthline.com/nutrition/high-cholesterol-foods. Imechukuliwa 12/4/2020
Web Md Food to eat. https://www.webmd.com/cholesterol-management/heart-health-foods-to-buy-foods-to-avoid. Imechukuliwa 12/4/2020
Health Harvard ,Food that lower cholesterol. https://www.health.harvard.edu/heart-health/11-foods-that-lower-cholesterol imechukuliwa 12/4/2020
Your guide to lowering your cholesterol with therapeutic lifestyle changes. National Heart, Lung and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/all-publications-and-resources/your-guide-lowering-cholesterol-therapeutic-lifestyle. Imechukuliwa 12/4/2020