top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Charles W, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Komamanga
Komamanga

Komamanga huwa na virutubisho vingi sana kama vile nyuzi lishe, Protini, Vitamin C, Vitamin K,Madini ya Folate, Potassium

Pia kuna kemikali aina mbalimbali kama punicalagins ambayo husaidia kuzuia magonjwa ya michomo ya chembechembe hai za mwili (antinflammatory) na magonjwa ya mwili kujishambulia wenyewe(autoimmune) ambayo huongoza kwa vifo kama vile Magonjwa ya moyo, kisukari aina ya 2, ugonjwa wa alzheimer. Hata hivyo unene pia unaweza kuzuia kwa kutumia tunda hili

Kuzuia saratani ya tezi dume

Tafiti zinaonyesha juishi ya komamanga huweza kuzuia kiwango cha kemikali ya PSA ambayo hutolewa na tezi dume kwa. Kemikali hii ikiwa inapozalishwa kwa wingi huweza kuishia chembe za tezi kuwa saratani. Kiwango cha PSA kikijiongeza mara mbili zaidi kwa mtu mwenye saratani hatari yake ya kufa huongezeka mara dufu zaidi

Katika tafiti zinaonyesha kwamba juisi ya komamanga kiasi cha Mililita 250 kwa siku ina uwezo wa kurudisha nyuma kujizalisha kwa kemikali hii mara mbili badala ya miezi 15 na kuwa miezi 54

Pia tunda hili linauwezo wa kuuza chembe zenye sifa ya saratani(apoptosis)

  • Kupunguza shinikizo la damu

  • Matumizi ya mililita 150 ya juisi ya komamanga kwa siku kwa mda wa wiki mbili imeonyesha kupunguza shinikizo la damu.

  • Kushusha Shinikizo la damu la juu

Shinikizo la damu la juu huweza kusababisha magonjwa ya mishipa ya damu na moyo, magonjwa haya huongoza katika kusababisha vifo vya ghafla

Magonjwa ya maungio ya mwili (baridi yabisi)

Juisi ya komamanga ina kemikali zinazoweza kupambana na magonjwa ya maungio ya mwili kama homa yabisi na maumivu ya maungio ya mwili

Uwezo huu umetokana na kuwa na kemikali zinazopambana dhidi ya michomo na kujishambulia kwa chembe za mwili

Kuua bakiteria na fungus hivyo huweza kusaidia kutibu magonjwa ya kinywa

Kutibu tatizo la kuishiwa kwa nguvu za kiume, uume kushindwa kusimama ama kuwa na matatizo ya kusimama

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:07:19
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Kandylis, et al. “Food Applications and Potential Health Benefits of Pomegranate and its Derivatives.” Foods (Basel, Switzerland) vol. 9,2 122. 23 Jan. 2020, doi:10.3390/foods9020122

bottom of page