Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Maharagwe
Zipo aina tofauti za maharagwe kama maharage ya soya na maharage ya kawaida
Faida za maharagwe
Maharage kwa ujumla ni chanzo kikubwa cha protini (soya huongoza) kutoka katika mimea, protini hii husaidia kujenga mwili.
Protini hii huweza kujenga mwili kama misuli, kusaidia kuziba/kupona kwa vidonda/majeraha ya mwili n.k
Maharage ya soya yamekuwa yakitumika kutengeneza uji wa lishe kwa ajiri ya watoto na watu wazima.
lishe hii huwa ina mchanganyiko wa maharage, karanga, ulezi ama mchele, na wengine huweka dagaa pia
Kwa kutumia mchanganyiko huu unapata mwili weye afya na akili safi.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Maharage
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Maharage
Maharage yana kemikali muhimu iitwayo Phenolic Acid.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100
Nishati = 334kcal
Mafuta = 1.1g
Maji = 11.75g
Kabohaidreti = 61g
Sukari = 2.1g
Nyuzilishe = 15g
Protini = 23g
Vitamini zinazopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100
Vitamini B1 = 0.068mg
Vitamini B2 = 0.215mg
Vitamini B3 = 2.110mg
Viatmini B5 = 0.780mg
Vitamini B6 = 0.397mg
Vitamini B9 = 394mcg
Vitamini C =4.5mg
Vitamini E =0.21mg
Vitamini K = 5.6mg
Madini yanayopatikana kwenye Maharage yenye gramu 100
Kalishiamu = 83mg
Kopa = 0.7mg
Floraidi = 2.2mg
Madini Chuma = 6.69mg
Magineziamu = 138mg
Manganaizi = 1.111mg
Fosifolasi = 406mg
Potashiamu = 1359mg
Sodiamu = 12mg
Zinki = 2.79mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Maharage
Hupunguza uzito usiotakiwa.
HKupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Hupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kupooza.
Huongeza kinga ya mwili na kusaidia ukuaji.
Huimarisha utendaji kazi wa moyo na kuzuia ugonjwa wa shinikizo la juu la damu.
Huimarisha utendaji kazi wa Ini.
Huongeza hamu ya kula.
Husaidia kwenye mchakato wa utengenezwaji wa chembe chembe nyekundu za damu.
Imeboreshwa,
21 Machi 2022, 20:16:27
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Polak, Rani et al. “Legumes: Health Benefits and Culinary Approaches to Increase Intake.” Clinical diabetes : a publication of the American Diabetes Association vol. 33,4 (2015): 198-205. doi:10.2337/diaclin.33.4.198
Beans .https://www.nutritionvalue.org/Beans%2C_raw%2C_mature_seeds%2C_red%2C_kidney_nutritional_value.html. Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.
Ganesan K., Xu B. Polyphenol-Rich Dry Common Beans (Phaseolus vulgaris L.) and Their Health Benefits. Int. J. Mol. Sci. 2017;18:2331. doi: 10.3390/ijms18112331. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7915747/. Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.
Rizkalla SW, Bellisle F, Slama G. Health benefits of low glycaemic index foods, such as pulses, in diabetic patients and healthy individuals. Br J Nutr. 2002 Dec;88 Suppl 3:S255-62. doi: 10.1079/BJN2002715. PMID: 12498625. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/12498625/. Imechukuliwa tarehe 20 January 2022.