Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Njegere
Njegere ni Chakula jamii ya mbegu,mbegu hizi huw katika kundi kubwa linaitwa legumin ambapo huwa na protini kwa wingi inayosaidia katika ukuaji wa mwili
Virutubisho
Vilivyomo ndani ya njegere hutegemea endapo njegere hiyo bado ni mbichi au ikiwa imekauka
Njegere mbichi
Huwa na viinirishi vifuatavyo,
Vitamin A
Vitamin K
Thiamine
Folate
Manganese
Madini ya fosforasi
Huwa na protini kwa wingi
Umuhimu wa Njegere mbichi
Matumizi mazuri ya mara kwa mara ya njegere huweza kusaidia katika kukinga ama kuupa mwili uwezo wa kupambana na hali na magonjwa mbalimbali, baadhi ya faida ni;
Hudhibiti kiwango cha sukari katika damu
Huimarisha mifupa
Huimarisha moyo
Huimarisha mmen'genyo wa chakula mwilini
Hukinga dhidi ya magonjwa sumu, Kama kisukari, Saratani na magonjwa ya moyo
Madhara ya njegere
Kama ilivyo kwamba kila kitu kina madhari kikitumiwa bila utaratibu mzuri, Njegere mbichi pia huweza kusababisha tumbo kujaa na gesi endapo zitatumiwa bila utaratibu maalumu. Kwa wagonjwa wa Vidonda vya tumbo hawashauriwi kutuumia chakula hiki.
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:04:01
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Grant J, Cooper P. Peas (Pisum sativum L.). Methods Mol Biol. 2006;343:337-45. doi: 10.1385/1-59745-130-4:337. PMID: 16988357.