Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. mangwella S, MD
Alhamisi, 18 Novemba 2021
Pera
Pera ni tunda linalopatinaka kwenye nchi zilizoko ukanda kitropiki. Kama ilivyo kwa matunda mengine, mapera pia yanaumuhimu kwenye mwili wa binadamu kama ambavyo wataalamu wa afya duniani kote wamekua wakisisitiza matumizi matunda kutokana na kuwa na wingi wa viinilishe vinavyopatinakana. Pera linaweza kutumika kama sharubati au kuliwa kama chakula.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye mapera
Sukari
Nyuzilishe
Mafuta
Protini
Vitamini
Madini
Kabohaidreti
Viinilishe vinavyopatikana kwenye mapera yenye gramu 100
Nishati = 68kacl
Protini = 2.55g
Sukari = 8.92g
Nyuzilishe = 5.4g
Kabohaidreti = 14.32g
Mafuta = 0.95g
Maji = 80.8g
Vitamini zinavyopatikana kwenye mapera yenye gramu 100
Vitamini A = 31ug
Vitamini B1 = 0.067mg
Vitamini B2 = 0.04mg
Vitamini B3 = 1.084mg
Vitamini B5 = 0.451mg
Vitamini B6 = 0.11mg
Vitamini B9 = 49ug
Vitamini C = 228.3mg
Vitamini K = 2.2ug
Madini yanayopatikana kwenye mapera yenye gramu 100
Kalishiamu = 18mg
Zinki = 0.23mg
Madini Chuma = 0.26mg
Magineziamu = 22mg
Manganizi = 0.15mg
Potashiamu = 417mg
Sodiamu = 2mg
Fosifolasi = 40mg
Faida za ulaji wa mapera kwenye mwili wa binadamu
Kinga nzuri dhidi ya kisukakari
Huimarisha uwezo wa kuona pamoja na ngozi
Huimarisha kiwango cha shinikizo la damu
Huimarisha afya ya akili na moyo
Huimarisha ngozi
Huimarisha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula
Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini
Hupunguza uzito
Imeboreshwa,
18 Novemba 2021, 08:38:59
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii