Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021
Pilipili manga
Huwa na radha ya mwasho kama pilipili, virutubisho vifuatavyo vinapatikana katika kiungo hiki
​
Madini chuma, sodiamu, kalisium, maganesi, zinki, chromium na vitamin A, vitamin C na virutubisho vingine kwa kiasi kidogo
Faida za pilipili manga
Huongeza ufyonzaji wa virutubisho kama vitamin A&C, selenium, karotini na virutubisho vingine.
Huimarisha umengenyaji wa chakula
Husisimua tezi zilizo kwenye kifuko cha chakula tumboni na kusababisha kuzalishwa tindikali kwa wingi , inayosaidia katika uvunjaji wa chakula na hivyo kuharakisha tendo la umengenyji wa chakula kikiwa tumboni. Matatizo mengi ya umengenyaji hutokana na ukosefu wa tindikali katika tumbo hivyo kiungo hiki huweza kutibu matatizo ya gesi tumboni, kiungulia, kushiba haraka, na choo kigumu. Tindikali hii pia huua bakiteria katika tumbo wanaoingia na chakula.
Huongeza hamu ya kula
Mbali na kuongeza radha ya chakula kiungo hiki pia huongeza hamu ya kula kwa kushinikiza mishipa ya fahamu ya puani. Kwa namna hii huweza kutumika kwa watu wanaopata shida ya kula.
Hupunguza uzito
Ingawa huongeza hamu ya kula, tafiti zinaonyesha gamba la nje la pilipili manga huwa na kemikali inaoitwa phytonutrient ambayo huongeza uvunjwaji wa chembe mafuta mwilini.
Hata hivyo huongeza hamu ya kukojoa, na kupumua haraka ambapo husaidia katika kuondoa sumu na maji mengi mwilini
Hupunguza gesi tumboni
Hupunguza utengenezwaji wa gesi na hupunguza kiwango cha gesi tumboni
Kama una gesi tumboni jaribu kutumia pilipili manga bada ka ya chili sorcce ama pilipili za unga
Kutibu tumbo kujaa ama kuvimbiwa unaweza kunywa glasi ya maziwa iliyochangaywa na pilipili manga.
Hufungua pua zilizozibwa na kamasi au mafua
Huvunja mafua kwenye pua na kusaidia kuondoa kuziba kwa pua, pia huwa na uwezo wa kupambana na bakteria na hivyo ndo maana huwa kwenye matibabu ya kukohoa na mafua baridi
​
Hutumia kutibu mafua
Kunywa glasi ya maji uvuguvugu iliyochanganywa na pilipili manga mara mbili ama tatu kwa siku kusafisha mfumo wa hewa
Njia nyingine ni kwa kuvuta mvuke wenye mchanganyiko wa pilipili manga na itasababisha upige chafya na kwa kufanya hivi mafua na njia za mfumo wa hewa zitakuwa safi.
Faida zingine
​
Huondoa maumivu ya maungio na michomo katika maungio ya mwili (arthritis)
Hupambana na saratani na magonjwa mengine kwa kuwa na antioxidant san asana saratani ya matumbo na titi, pia hupambana na shinikizo la juu la damu kisukari na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Hutibu msongo wa mawazo
Kiungo hiki huongeza uzalishaji wa homoni ya serotonin ambayo huwa na umuhimu katika mfumo wa fahamu kwa kusaidia katika kuimarisha hali ya mtu. Kiasi kidogo cha serotonin husababisha msongo wa mawazo(huzuniko) kwa binadamu. Hata hivyo huongeza kiasi cha kemikali asili za endorphine zinazopooza maumivu katika mwili na kuimarisha hali ya mtu. Hupunguza msongo wa mawazo na kukufanya ujihisi vema na mwenye afya. Huongeza ufahamu wa mambo.
Hutibu magonjwa ya fizi
Kama harufu mbaya kinywani na michomo katika fizi
Huongeza uzalishaji wa maziwa kwa wamama wajawazito
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:03:51
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Butt MS, et al. Black pepper and health claims: a comprehensive treatise. Crit Rev Food Sci Nutr. 2013;53(9):875-86. doi: 10.1080/10408398.2011.571799. PMID: 23768180.
Vijayakumar RS, et al. Antioxidant efficacy of black pepper (Piper nigrum L.) and piperine in rats with high fat diet induced oxidative stress. Redox Rep. 2004;9(2):105-10. doi: 10.1179/135100004225004742. PMID: 15231065.