Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sima A, CO
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 2 Aprili 2020
Vitamin E
Vitamini E ni miongoni mwa vitamini inayoweza kuyeyusha Mafuta. Kuna aina nyingi za vitamini E, aina mojawapo muhimu kwa binadamu ni Vitamin E aina ya alpha-tocopherol.
Vitamini E hufanya kazi kama antioksidanti, kazi za ki antioksidanti ni kuzuia uharibifu wa seli kutokana na elekroni huru zinazoambaa mwilini kutoka kwenye matokeo ya uchakataji wa chakula na sumu shughuli mbali mwilini.
Kazi nyingine ni kuimarisha kinga za mwili na husaidia kuzuia kusongamana kwa damu kwenye mishipa ya moyo.
Vitamini E husaidia kudumisha uimara wa Ngozi, macho na kuimarisha ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa ya kuambukizwa.
Vitamini E ni kirutubisho ambacho kinahitajika mwilini ili kusaidia kuzaliwa upya kwa seli.
Vitamin E inajulikana sana kwa faida zake kwenye afya ya ngozi na macho, kwa kuyapa uwezo wa kuona na kufanya Ngozi kuwa imara yenye mwonekano mzuri. Vitamini E hupatikana kwa asili katika vyakula vingi na pia huweza kuongezwa kwenye vyakula.
Vyanzo vya Vitamin E
Mbegu za maboga
Mbegu za alizeti
Mchicha
Pilipili nyekundu
Matunda na mboga za majani
Mafuta ya mimea - kama vile soya, mahindi, karanga na mbegu
Nafaka na bidhaa za nafaka
Mafuta ya mboga
Mboga za majani
Nyama ya nguruwe
Karanga, siagi ya karanga
Ishara za Upungufu
Kwa sababu vitamini E hupatikana kkwenye aina kadhaa za vyakula na virutubisho. Watu ambao wana shida kwenye utumbo au wana magonjwa mbalimbali (mfano shida ya kongosho, Fibrosisi ya sistiki) wanaweza kupata upungufu wa vitamini E.
Zifuatazo ni ishara za kawaida za upungufu:
Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati au mtoto njiti au mtoto kuzaliwa na uzito kidogo (chini ya gramu 1,500)
Misuli kuwa dhaifu
Magonjwa ya moyo
Saratani
Magonjwa yanayohusiana na umri
Kuona hafifu
Uharibifu wa macho
uharibifu wa mishipa ya damu ya miguuni na mikononi
Inafanyaje kazi?
Vitamini E ni vitamini muhimu inayohitajika kwa utendaji sahihi wa viungo vingi mwilini, pia hufanya kazi za ki antioksidanti.
Kiasi cha vitamini E kinachopendekezwa mwilini.
Inapendekezwa kuwa wanaume na wanawake wenye umri wa miaka 14 na zaidi wanatakiwa kupata kiasi cha miligramu 15 cha vitamini E kila siku. Kiwango hiko kinajumlisha wanawake wajawazito.
Wanawake wanaonyonyesha wanahitaji kidogo chenye vitamin nyingi Zaidi kwa kupata angalau miligramu 19 cha vitamin E kila siku.
Ni muhimu kupata vitamini E inayohitajika mwilini kutoka kwenye chakula unachokula kila siku. Mwili wako huwa na uwezo wa kuhifadhi vitamin E kwa matumizi ya baadaye.
Madhara ya Kiwango kikubwa cha vitamin E mwilini
Hakuna ushahidi wa kutosha kujua nini na athari gani unaweza pata endapo utatumia kwiango kikubwa cha vitamin E.
Faida ya Vitamini E
Kulainisha ngozi
Inasaidia kuponya vidonda
Hukinga Ngozi namaradhi
Huounguza miwasho ya ngozi
Kuzuia au kupunguza mwonekano wa makovu
Hukinga Ngozi na mionzi ya jua
Huimarisha kucha
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:05:17
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Overview Information of Vitamin E.(https://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-954/vitamin-e#). imechukuliwa 03/04/2020
Vitamin E- Fact Sheet for Health Professionals. https://ods.od.nih.gov/factsheets/VitaminE-HealthProfessional/.imechukuliwa 03/04/2020
Vitamin E — Written by Kathryn Watson,Medically reviewed by Cynthia Cobb, DNP, APRN on March 7, 2019.https://www.healthline.com/health/vitamin-e-for-face#other-products-and-uses.imechukuliwa 03/04/2020
THE NUTRITION SOURE Vitamin E Harvard.https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/vitamin-e/.imechukuliwa 03/04/2020
Vitamins and minerals - Vitamin E. https://www.nhs.uk/conditions/vitamins-and-minerals/vitamin-e/.imechukuliwa 03/04/2020
Benefits of vitamin E — Written by Zawn Villines,Medically reviewed by Debra Rose Wilson, PhD, MSN, RN, IBCLC, AHN-BC, CHT on January 29, 2020.https://www.medicalnewstoday.com/articles/318168#Risks-and-considerations.imechukuliwa 03/04/2020