top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sima A, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Jumatano, 6 Mei 2020

Vyakula vyenye kolestro kwa wingi
Vyakula vyenye kolestro kwa wingi

Kolestro ni mafuta muhimu kwenye chembe hai ya mwili wa binadamu yanayopatikana pia kwenye mimea na wanyama wengine na kwa jina jingine hufahamika kama lehemu. Licha ya kuwa na umuhimu mkubwa kama vile kutengeneza homon mwilini, mafuta haya yanapozidi mwilini hupelekea kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.


Vyakula vyenye kolestro kwa wingi;


  • Maya:- Yai moja huweza kuwa na kiwango cha miligramu 211 za kolestro

  • Nyama za ogani:- kama moyo na maini huwa na kolestro kwa wingi

  • Vyakula vya kukanga:- kama kuku huwa na mafuta wa wingi ya kolestro

  • Nyama za kusindikwa

  • Keki, yogati n.k

  • Samaki wenye magamba:- kama kaa na shrimp- Samaki hawa huwa na mafuta kwa wingi kuliko samaki wengine

  • Maziwa mgando:- haya ni maziwa yaliyoganda ambayo hujitengenezea mafuta yake na kuwa na kolestro kwa wingi

  • Jibini

  • Blueband

  • Nyama nyekundu huwa na kolestro nyingi zaidi kuliko nyama nyeupe



Vyakula vyenye kolestro kidogo


  • Mimea na mbegu jamii ya mboga za kunde- Kama maharage,kunde na mbaazi

  • Aina nyingi sana za matunda mfano parachichi, chungwa n.k

  • Samaki mfano aina ya salmon

  • Maharage ya soya

  • Mboga za majani

  • Majani ya mboga za kijani


Walio hatarini kuwa na kolestro kwa wingi kwenye damu


Umri mkubwa Zaidi:- kadri umri unavyozidi kuwa mkubwa Zaidi kiwango cha kolestro mwilini huongezeka. Watoto wadogo na vijana huwa na kiwango kidogo cha kolestro


Hali ya kurithi:- Kiwango kinakuwa kikubwa kati yaw ana familia wa damu moja.


Kuwa na uzito kupita kiasi:- Kuwa na uzito kupita kiasi huweza kuongeza kiasi cha kolestro mwilini kwa kuwa kiasi hiko huchangiwa na Mafuta.


Asili:- watu asili ya Afrika(watu weusi) wengi huwa na kiwango cha juu cha kolestro mwilini.



Njia za kiafya za kuepuka kolestro kwa wingi


  • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa wingi kama matunda ,maharage, kunde,

  • Kufanya mazoezi kwa wingi

  • Kupunguza uzito

  • Kuacha tabia zisizo za kiafya kama kula vyakula vya mafuta sana

  • Kula matunda kwa wingi


Magonjwa yanayotokana na kiwango kikubwa cha kolestro kwenye damu


  • Shinikizo la juu la damu ( presha ya kupanda)

  • Kisukari

  • Mshituko wa moyo

  • Kuferi kwa moyo

  • Kiharusi

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:08:45
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

bottom of page