Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Alhamisi, 9 Aprili 2020
Faida za kiafya za madini ya Iodine
Ni aina ya madini yanayopatikana kwenye mboga za majani haswa zile zinazolimwa kwenye udongo na kando kando ya maji ya bahari.
Ni muhimu kupata madini ya iodine kwenye chakula maana husaidia mfumo wa homoni kufanya kazi vizuri na watoto kukua
Vyakula vyenye wingi wa Iodine:
Mbogamboga za baharini
Aina ya samaki anaiyeitwa Cod
Maziwa na bidhaa zinazotokanana vito maziwa
Chumvi ya iliyoongezewa madini haya
Kiumbe anayeitwa kamba
Mayai
Faida za iodine
Huwezesha tezi ya thairoidi kuzalisha homoni zake
Hukinga mwili dhidi ya tatizo la goita
Huthibiti utendaji kazi mkubwa kupita kiasi wa tezi ya thairoidi
Hutibu saratani ya tezi ya thairoidi
Husaidia ukuaji mzuri wa mishipa ya fahamu ya mtoto akiwa tumboni mwa mama
Husaidia uwezo mzuri wa akili kufanya kazi
Husaidia kuimarisha uzito wa mtoto mchanga
Hutumika kuua vijidudu kwenye maji na kuyafanya salama kwa ajili ya kutumika
Kutibu Maambukizi ya bakteria
Humkinga mtoto tumboni dhidi ya magonjwa ya mfumo wa fahamu kama mgongo wazi n.k
Dalili za upungufu wa Iodine
Kuonekana kwa uvimbe wa tezi ya thairoidi ikijulikana kama Goita
Maumivu kwenye tezi ya thairoidi
Kupumua kwa shida
Kumeza kwa shida
Mwili kuchoka sana ku
Mapigo ya moyo kwenda ndivyo sivyo
Kuhisi baridi sana
Kutoota kwa nywele
Kuwa na huzuni
Kupata uzito mkubwa kwa ghafla
Maudhi ya Iodine
Kichefuchefu au kutapika
Kuharisha
Homa
Kuhisi hali ya kuchomwa kwenye koo na mdomoni
Maumivu ya tumbo
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:06:02
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
HealthLineIodineDeficienyhttps://www.healthline.com/nutrition/iodine-deficiency-symptoms 8/4/2020. Imechukuliwa 8.04.2020
WebMdIodinehttps://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-35/iodine 8/4/2020. Imechukuliwa 8.04.2020
NIH. Iodine. https://ods.od.nih.gov/factsheets/Iodine-HealthProfessional/. Imechukuliwa 8.04.2020
MedicalNewTodayIodinehttps://www.medicalnewstoday.com/articles/288471. Imechukuliwa 8.04.2020