Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 10 Aprili 2020
Faida za Ngano mwilini
Ngano ni moja ya zao linalotumika sana na binadamu ulimwenguni, huvunwa kutoka kwenye mmea wa majani unaitwa triticum ambao huota kwnye maeneo mbalimbali duniani.
Matumizi ya ngano huwa mengi sana, mfano tu ni kutengeneza unga wa mikate, keki, chapati na mandazi. Unga wa ngano una protini inayofahamika kwa jina la gluteni, protini hii husaidia kuimarisha kinga ya mwili .
Hata hivyo baadhi ya watu huwa na mzio na protini hii, mara wanapokula huharisha au kuumwa tumbo. Watu wenye ugonjwa wa Crohn wanashauriwa kuepuka vyakula vya ngano kutokana na kuwa na protini hii.
Aina za ngano
Kitiba, kuna aina mbili za ngano ambazo ni;
a.Ngano isiyokobolewa
Hii ni ile ambayo haijatolewa ganda lake na ni ya rangi ya kahawia ,hii ina virutubisho vyote asilimia 100
b.Ngano illiyokobolewa
Hii huonekana kama unga wenye rangi nyeup, kukoboa ngano inapunguza baadhi ya virutubisho
Virutubisho vya ngano
Nishati
Protini
Wanga
Sukari
Nyuzinyuzi
Mafuta
Madini ya selenium, manganezi, fosforazi, shaba na foleti
Vitamin B6 na B12
Faida za ngano
Ngano iliyoandaliwa kutoka kiwandani huwa na sukari ndogo inayoweza kutumika hata kwa wagonjwa wa kisukari
Huongeza nyuzilishe ambazo huongeza uzito wa kinyesi na kufanya kipite kirahisi na pia baadhi yake hushambulia bakteria
Husaidia mwili katika kuwa na wingi wa protini ,ngano ina asilimia 80 ya protini ,
Ni chanzo kizuri cha madini Kama selenium, manganese, phosphorus, copper na folate
Ni chanzo kizuri cha Vitamin kama vitamin B6 ,Vitamin B12,
Hupunguza hatari ya saratani ya utumbo mwembamba kwa kuwa na antioksidanti ambazo ni ferulic, phytic, Alkylresorcinols,lutein ,lignans
Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo
Hupunguza hatari ya kupata utapiamlo
Hutia mwili nguvu kwa kuwa huwa na wanga
Huzuia hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari
Huepusha hatari ya kupata mawe kwenye figo
Huzuia pumu kwa watoto wadogo
Hupunguza dalili kukoma kwa hedhi
Huimarisha afya ya nywele
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:15:58
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 280.
Health Line Wheat. https://www.healthline.com/nutrition/foods/wheat Imechukuliwa 10/4/2020
Organic Facts Wheat. https://www.organicfacts.net/health-benefits/cereal/wheat.html Imechukuliwa 10/4/2020
Whole grain. https://wholegrainscouncil.org/whole-grains-101/whole-grains-101-orphan-pages-found/health-benefits-wheat Imechukuliwa 10/4/2020
Whfoods Wheat. http://www.whfoods.com/genpage.php?tname=foodspice&dbid=66 Imechukuliwa 10/4/2020