Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021
Forosadi
Forosadi ni matunda madogo yanayopatina kwenye familia ya beri (beri nyeusi na beri ya bluu), na huwa na rangi tofauti kama ilivyo kwenye picha, forosadi rangi ya blue na nyekundu, matunda haya huwa na kiwango kikubwa cha viini vya anthocyanins ambayo imeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo.
Mforosadi hulimwa kwa wingi huko Asia ya kusini,Ulaya ,Afrika ya kusini,Amerika ya kusini na Amerika Kaskazini na hupatikana kwenye masoko na maeneo mengi duniani.Kama ilivyo kwa matunda mengine, Forosadi pia ni muhimu kwa afya kwa sababu ya uwepo wa viinilishe na virutubisho.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye forosadi
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Mafuta
Protini
Vitamini
Madini
Maji
Sukari
Viinilishe vinavyopatikana kwenye forosadi zenye gramu 100
Nishati = 43kcal
Sukari = 8.1g
Protini = 1.4g
Nyuzilishe = 1.7g
Kabohaidreti = 9.8g
Mafuta = 0.4g
Maji = 87.7g
Vitamini zinazopatikana kwenye forosadi zenye gramu 100
Vitamini A = 1mcg
Vitamini B1 = 0.029mg
Vitamini B2 = 0.101mg
Vitamini B3 = 0.62mg
Vitamini B6 = 0.05mg
Vitamini B9 = 6mcg
Vitamini C = 36.4mg
Vitamini E = 0.87mg
Vitamini K = 7.8mcg
Madini yanayopatikana kwenye forosadi zenye gramu 100
Kalishiamu = 39mg
Sodiamu = 10mg
Zinki = 0.12mg
Potashiamu = 194mg
Fosifolasi = 38mg
Magineziamu = 18mg
Madini Chuma = 1.85mg
Faida za forosadi
Faida za kiafya zitokanazo na forosadi
Kurekebisha na kuimarisha kiwango cha sukari mwilini
Kupunguiza hatari yakupatwa na Kansa
Kupunguza rehemu(kolestro)
Kuimarisha na Kupunguza hatari ya kupatwa magonjwa ya moyo
Kuimarisha afya ya Kongosho hivyo kupelekea kuzuia ugonjwa wa kisukari
Forosadi kwenye tafiti
Tafiti zinaonyesha kwamba kutumia juisi ama tunda hili kwa kiwango kinachotakiwa kunaweza kusababisha kupunguza shinikizo la damu, kutunza kuta za ndani za mishipa ya damu.
Utafiti uliofanyika karibuni umeonyesha kwamba wanawake wanaokula ama kunywa glasi tatu au zaidi za juisi ya forosadi hupunguza kwa asilimia 34 zaidi kupata magonjwa ya moyo (kushikwa kwa moyo) na mishipa ya damu.
Haijarishi ni rangi gani ya forosadi utumie, kila aina ya tunda hili huwa na madini/viinirishe vya kufana
Forosadi pia hupunguza kiwango cha kolestro na uzito mkubwa
Soma namna ya kuandaa kifungua kinywa cha matunda ya forosadi kwa kubonyeza hapa
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 15:15:26
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
H Zhang, et al. Effects of Mulberry Fruit (Morus alba L.) Consumption. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5981255/. Imechukuliwa 22.10.2021
Ma Z.F., Zhang H. Phytochemical constituents, health benefits, and industrial applications of grape seeds: A mini-review. Antioxidants. 2017;6:71.
Veeresham C. Natural products derived from plants as a source of drugs. J. Adv. Pharm. Technol. Res. 2012;3:200–201. doi: 10.4103/2231-4040.104709.
Zhang H., Ma Z.F. Phytochemical and pharmacological properties of Capparis spinosa as a medicinal plant. Nutrients. 2018;10:116.
https://uc.xyz/14LBMi?pub=link [Effects of Mulberry Fruit ( Morus alba L.) Consumption on Health Outcomes: A Mini-Review - PubMed]Imepitiwa tarehe 29/11/2021