top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Charles W, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Kungu
Kungu

Kungu ni tunda linalopatikana sana barani afrika, kuna aina tofauti za kungu, aina hizi hutokana na asili ya mmea unaotoa tunda hilo na sehemu mmea huo ulipo. Karanga ya tunda la Kungu imekuwa ikifanyiwa tafiti nyingi sana na hii ni kutokana na faida zake nyingi katika mwili wa binadamu. Tunda hili kwa kuwa lina vitamin na virutubisho vyenye mchango mkubwa ndani ya mwili wa binadamu limekuwa likitumika kama dawa kwa ajili ya hali na magonjwa mbalimbali


Virutubisho ndani ya kungu


Karanga ya Kungu huwa na virutubisho vifuatavyo ndani yake;


  • Protini

  • vitamin E

  • nyuzinyuzi

  • mafuta mazuri

  • madini kalisi

  • madini ya magnesium


Kungu huwa na nini ndani ya mbegu zake?

Kulingana na tafiti dhidi ya mbegu ya kungu, virutubisho na vitamin zifuatazo hupatikana katika tunda la kungu, kumbuka vilivyomo vimezingatia mbegu 23 za kungu

  • gramu 6 za protini

  • gramu 7.3 za vitamin E

  • gramu 4 za nyuzinyuzi

  • gramu 13 za mafuta mazuri

  • miligramu 200 za madini kalisi

  • miligramu 77 za madini ya magnesium


Faida zakiafya za kungu

Zipo faida nyingi sana za karanga ya tunda la kungu, faida hizo hutokana na virutubisho vilivyomo ndani ya tunda hilo, faida zifuatazo huwa miongoni mwa faida nyingi za tunda karanga ya tunda hili.

​

  • Huupa moyo afya njema kwa kupunguza lehemu mbaya katika mfumo wa damu na kuongeza lehemu nzuri mwilini, hivyo hukuweka salama dhidi ya magonjwa ya moyo yatokanayo na mafuta mabaya ndani ya mwili

  • Michomo na mafuta kujaa chini ya tumbo( kitambi)- karanga ya tunda la kungu hupunguza michomo kwenye mwili na kukupa na hivyo kukusababishia kupunguza vihatarishi vya kupata magonjwa ya moyo, pia tafiti zinaonyesha kuwa kwa kula karanga hizi hupunguza uzito wa kupita kiasi na mafuta yanayatuama katika tumbo yanayosababisha kitambi.

  • Hupunguza sukari katika damu- kwa tafiti zilizofanyika imeonekana karanga hizi huwa na uwezo wa kupunguza sukari mwilini kwa mgonjwa wa kisukari na mgonjwa asiye na kisukari hivyo huwa mbadala mzuri kutumika kwa mgonjwa wa kisukari katika kupambana na kupanda kwa sukari katika damu. Hata hivyo mtu ambaye hana kisukari anaweza tumia karanga hizi katika kuweka mwili kuwa sawa na kuzuia vihatarishi vya kupata kisukari.

  • Hupunguza uzito

  • Hupunguza shinikizo la damu- madini ya kali huwa na mchango mkubwa katika kupunguza shinikizo la damu mwilini, hivyo kwa mtu anayekula matunda hayo katika milo yeke anajiondoa katika hatari ya kupata shinikizo la damu mwilini mwake.

Imeboreshwa,
29 Novemba 2021, 05:28:46
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

bottom of page