Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
Jumapili, 12 Aprili 2020
Mboga za majani
Mboga za majani ni muhimu kwenye mlo kamili wa binadamu, huwa vitamini, madini na nyuzinyuzi kwa wingi na kalori kidogo.
Mboga hizi huweza kuliwa zikiwa mbichi kama saladi au kupikwa kwenye
Ulaji wa mboga za majani una faida kubwa sana katika mwili wa binadamu kama vile; kupunguza uzito mkubwa kupita kiasi- (obeziti), magonjwa ya moyo na pia shinikizo la juu la damu.
Makundi au aina za mboga
Mboga za majani za majani mfano; kabichi, spinachi, mchicha, mlenda, majani ya maboga, kisamvu, matembel, figiri, mchunga.
Mboga za majani za mizizi mfano; karoti, vitunguu, viazi vitamu, viazi mviringo
Mboga za majani za matunda mfano; nyanya, bamia, hoho, maboga
Mboga za majani za maua mfano; brokoli,
Faida za mboga za majani
Husaidia kuongeza kinga ya mwili kwa sababu ya kuwa na vitamin kwa wingi sana, hasa vitamin A (mboga zote zenye rangi ya njano na nyekundu), vitamin C (mbogamboga zenye rangi ya kijani) na vitamin K (mfano ni spinach)
Husaidia kuongeza kiwango cha vimeng’enya kwa ajili ya mmeng’enyo wa chakula
Kwa kuwa mboga nyingi zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi ambazo husaidia tumbo kutojaa gesi, kuzuia choo kigumu/konstipesheni na huongeza virutubisho mwilini.
Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini
Husaidia kuongeza kinga ya mwili
Kwa sababu ya kuwa na vitamin kwa wingi sana, hasa vitamin A (mboga zote zenye rangi ya njano na nyekundu), vitamin C (mbogamboga zenye rangi ya kijani) na vitamin K (mfano ni spinach)
Husaidia kuongeza kiwango cha vimeng’enya
Kwa kuwa mboga nyingi zina kiwango kikubwa cha nyuzinyuzi ambazo husaidia tumbo kutojaa gesi, kuzuia choo kigumu/konstipesheni na huongeza virutubisho mwilini.
Hurekebisha kiwango cha sukari mwilini
Ulaji wa mboga za majani katika kila mlo husaidia sana katika kurekebisha kiwango cha sukari mwilini. Hii hutokana na kufyonzwa kwa kiasi kidogo cha chakula kinacholiwa na mboga za majani.
Huongeza chembe nyekundu za damu na husafisha damu
Kutokana na kiwango kikubwa cha kalisiamu kinachopatikana kwenye mboga ambacho husaidia kuimarisha mifupa.
Husaidia kutopungukiwa maji
Mwilini kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya sodiamu ambayo hutunza maji mwilini
Hupunguza msongo wa mawazo
Kwani mboga zina foliki asidi ambayo husaidia kurekebisha hali ya moyo.
Huimarisha ngozi baadhi ya mboga
Zina kemikali za beta karotini(mfano karoti) ambayo husaidia kufanya ngozi nyororo, na pia hutumika kama kinga ya ngozi dhidi ya jua.
Inasaidia tumbo kutokujaa gesi
Kwa kuwa mboga zina potasiamu na madini ambayo husaidia kurekebisha kiwango cha maji mwilini na sodiam ambayo hupambana dhidi ya gesi tumboni. Hata hivyo ulaji wa mboga za majani kwa wingi huweza kusababisha matatizo ya tumbo kujaa gesi.
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:14:07
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Concept of green vegetables concerning definition and types of green vegetable at https://blog.mybalancemeals.com/healyh/healthy eating/15 tasty -green -vegetables. Imechukuliwa11/4/2020
Betther healthchannel. Fruits and vegetables.https://www.betterhealth.vic.gov.au/health/healthyliving/fruit-and-vegetables. Imechukuliwa 11/4/2020
Concept of green vegetables about benefits at https://www.healthline.com/nutrition/leafy-green-vegetables. Imechukuliwa 11/4/2020
V8.9 Health benefit of green vegetables. https://v8juice.co.uk/blog/9-health-benefits-of-green-vegetables. Imechukuliwa 11/4/2020