top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Dkt. Helen L, MD

Jumapili, 11 Juni 2023

Vyakula vya Protini
Vyakula vya Protini

Protini imeundwa kwa mnyororo wa amino asidi ziliounganishwa kwa pamoja na kiungo α-peptide na ni moja ya kirutubisho kinachohitajika kwa ajili ya ukuaji wa mwili, ukarabati wa tishu, na uzalishaji wa homoni na vimeng’enya vya mwili.


Protini hufahamika kama kijenzi cha mwili kwa sababu inahusika katika kujenga misuli, mifupa, ngozi, na seli nyingine muhimu.


Katika bara la Afrika, kuna vyanzo mbalimbali vya protini vinavyotokana na mimea na wanyama. Ingawa protini ni muhimu kwa afya, ulaji wa kiasi kingi au kidogo kupita kiasi unaweza kuwa na madhara kwa mwili. Makala hii imezungumzia kuhusu vyakula vyenye protini.

 

Vyanzo vya Protini ni vipi?

Kiwango cha protini kwenye chakula hutegemea aina ya chakula. Kwa ujumla, wanyama huwa ni chanzo kikuu cha protini ukilinganisha na vyakula vya mimea.

 

Vyanzo vya protini kutoka kwa wanyama na mazao yao

Vifuatavyo ni vyanzo vya protini kutoka kwa viumbe hai

  • Nyama – Ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, na wanyama poli n.k

  • Samaki na dagaa – Samaki wa baharini na wa maji baridi kama tilapia, sangara, na dagaa n.k

  • Mayai – Hutumika sana kama chanzo cha protini nafuu na rahisi kupatikana.

  • Maziwa na bidhaa zake – Kama vile mtindi, jibini, na siagi ya maziwa kutoka kwa ng’ombe, mbuzi, au ngamia.

  • Kuku na ndege wa mwituni – Kama vile kuku wa kienyeji, bata, na kware.

  • Panzi na wadudu wa kula – Wadudu kama senene na kumbikumbi ni chanzo kizuri cha protini.

Vyanzo vya protini kutoka kwenye mimea

Baadhi ya mimea kama vile aina ya kunde kama vile maharagwe, mbaazi na kunde huwa na kiwango kizuri cha protini.

 

Protini ya mimea jamii ya kunde hukosa protini aina ya methionine.

  • Maharagwe – Maharagwe mekundu, njano, na aina nyinginezo.

  • Njugu na karanga – Karanga, njugu mawe, mbegu za maboga, na alizeti.

  • Choroko, mbaazi na kunde – Ni vyanzo muhimu vya protini katika Afrika Mashariki na Magharibi.

  • Nazi na mbegu za maboga – Hutoa protini na mafuta yenye afya.

  • Nafaka zenye protini nyingi – Kama vile ulezi, mtama,

 

Kazi za protini

Protini huhitajika katika ukuaji wa mwili na kuponya tishu zilizoumia.


Madhara ya ulaji wa protini kidogo kupita kiasi


Ili kuepuka madhara yafuatayo, ni muhimu kula protini kwa kiasi kinachofaa na kuhakikisha mlo wako una uwiano mzuri wa virutubisho vingine muhimu kama vile wanga, mafuta yenye afya, vitamini, na madini. Kabla ya kufanya mabadiliko makubwa katika lishe yako, inashauriwa kushauriana na mtaalamu wa afya au lishe ili kuhakikisha mahitaji yako ya kiafya yanatimizwa ipasavyo. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya ulaji wa protini nyingi kupita kiasi.


1. Magonjwa ya figo

Ulaji mwingi wa protini unaweza kuongeza mzigo kwenye figo, hasa kwa watu wenye matatizo ya figo yaliyopo tayari. Hii inaweza kuharakisha kushindwa kufanya kazi kwa figo.


2. Upungufu wa Maji Mwilini

Kimeng'enya protini kinahitaji matumizi ya maji zaidi, na ulaji mkubwa wa protini bila kuongeza unywaji wa maji unaweza kusababisha upungufu wa maji mwilini.


3. Ukosefu wa Usawa wa Virutubisho

Kuzingatia sana ulaji wa protini kunaweza kupunguza ulaji wa vyakula vingine muhimu kama vile mboga mboga na matunda, na kusababisha upungufu wa nyuzinyuzi, vitamini, na madini muhimu.


4.Ongezeka la urea kwenye damu

Ulaji mwingi wa protini unaweza kuongeza viwango vya nitrojeni ya urea katika damu, ambayo inaweza kuashiria matatizo ya figo au upungufu wa maji mwilini.


5. Magonjwa ya Moyo

Baadhi ya vyakula vya protini, hasa nyama nyekundu na bidhaa za maziwa yenye mafuta mengi, vinaweza kuongeza viwango vya lehemu mbaya mwilini, na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo.


Madhara ya ulaji wa protini kidogo kupita kiasi


Ni muhimu kuhakikisha unapata protini ya kutosha katika mlo wako kupitia vyakula vilivyoorodheshwa katika makala hii. Kiasi kinachohitajika hutegemea umri, jinsia, na kiwango cha shughuli za mwili. Kujadili mahitaji yako ya protini na mtaalamu wa afya au lishe kunaweza kusaidia kupanga mlo unaofaa kwa afya yako. Upungufu wa protini unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya ikijumuisha matatizo yafuatayo:


1. Uvimbe.

Upungufu wa protini unaweza kusababisha uvimbe, hasa katika tumbo, miguu, na mikono. Hii ni kwa sababu protini kama albamini husaidia kuzuia mkusanyiko wa maji kwenye tishu.


2. Mabadiliko ya Mhemko

Neurotransmita, ambazo ni kemikali zinazotumiwa na ubongo kuwasiliana kati ya seli, nyingi hutengenezwa kutoka kwa amino asidi, ambazo ni sehemu za protini. Ulaji mdogo wa protini unaweza kuathiri uzalishaji wa neurotransmita, na hivyo kusababisha mabadiliko ya mhemko kama huzuni au hasira.


3. Masuala ya Nywele, Kucha, na Ngozi

Protini kama elastini, kolajeni, na keratini ni muhimu kwa afya ya nywele, ngozi, na kucha. Upungufu wa protini unaweza kusababisha ngozi kavu, nywele dhaifu au zinazokatika, na kucha zenye mipasuko.


4. Uchovu na Udhaifu

Kukosa protini ya kutosha kunaweza kuathiri misuli, na kusababisha udhaifu na uchovu. Pia, upungufu wa protini unaweza kusababisha upungufu wa damu, hali inayofanya mtu kujisikia mchovu zaidi.


5. Udumavu

Kwa watoto, upungufu wa protini unaweza kusababisha ukuaji hafifu wa mwili na akili, hali inayojulikana kama udumavu. Hii inaweza kuathiri ukuaji wao kwa maisha yote.

Imeboreshwa,
9 Machi 2025, 08:41:09
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Institute of Medicine. Protein and amino acids. In: Dietary reference intakes for energy, carbohydrate, fiber, fat, fatty acids, cholesterol, protein and amino acids. Washington (DC): Institute of Medicine, National Academies Press; 2005. p. 589–768.

  2. Dasgupta M, Sharkey JR, Wu G. Inadequate intakes of indispensable amino acids among homebound older adults. J Nutr Elderly 2005;24:85–99.

  3. FAO. Dietary protein quality evaluation in human nutrition. Report of an FAO Expert Consultation. FAO Food and Nutrition Paper No 92; FAO: Rome; 2013.

  4. Marinangeli CPF, House JD.. Potential impact of the digestible indispensable amino acid score as a measure of protein quality on dietary regulations and health. Nutr Rev 2017;75:658–67.

  5. Phillips SM. Current concepts and unresolved questions in dietary protein requirements and supplements in adults. Front Nutr 2017;4:13.

bottom of page