top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Charles W, MD

Dkt. Benjamin L, MD

Jumapili, 19 Aprili 2020

Vyakula vyenye Wanga
Vyakula vyenye Wanga

Wanga ni virutubisho vinavyo hitajika na mwili kwa ajili ya kuzalisha nishati ya mwili na hivyo kuupa mwili nguvu. Kuna vyakula vingi vya wanga katika jamii zetu na ndilo kundi la virutubisho vinavyopatikana kwa wingi ukilinganisha na makundi mengine ya virutubisho.


Vyakula vya wanga ni pamoja na nafaka kama vile mchele, mtama, mahindi, mihogo, viazi mviringo, viazi vitamu, asali na matunda yenye sukari. Vile vile tunapata wanga kwenye vyakula vya viwandani kama vile biskuti, soda juice, pipi, keki n.k


Kazi ya wanga mwilini


Kazi kubwa ya wanga ni kuupa mwili nguvu kwa kuzalisha nishati inayotoka kwenye glukosi. Ubongo hutegemea sukari ya glukosi inayotokana na wanga ili kufanya kazi vema. Pia wanga huvunjwavunjwa kua aina sukari inayounda vinasaba(DNA) saba vya binaadamu


Upungufu wa wanga mwilini


Watoto ndio kundi linalo athirika zaidi kutokana na upungufu wa wanga mwilini ijapokua watu wazima nao huathiriwa. Watoto wanapokosa wangamwlini huweza kupata utapiamlo wa marasmusi


Dalili za upungufu wa wanga


Kudumaa kiakili na mwili

Kukonda na kupungua uzito

Ngozi kusinyaa na kukunjamana, mtoto huonekana kuwa amezeeka

kuhara kunaweza kukawepo.

Kutopata choo/Konstipesheni

Mwili kuishiwa nguvu na kupelekea kuzimia au kuchanganyikiwa

Maumivu na kukakamaa kwa misuli wakati wa kazi ama mazoezi


Wanga kupita kiasi mwilini


Ingawa wanga ni muhimu sana mwilini, sio vizuri ukazidi kupita kiasi mwili. Kuzidi kwa wanga mwilini hutokana na kutokula mlo kamili, au kwa kula vyakula vya wanga peke yake kwa muda mrefu.


Madhara ya kuzidi kwa wanga


Kuongezeka uzito


Wanga nayozidi mwilini hubadilishwa kuwa mafuta na kuhifadhiwa sehemu mbalimbali za mwili. Hii huweza kuchangia uzito kupita kiasi.


Kuongeza atari ya ugonjwa wa sukari katika umri mkubwa


Vyakula vya wanga kwa wingi huchochea kongosho kuzalisha homoni ya insulin kwa wingi ili kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu. Baada ya muda mrefu kongosho huweza kuchoka na kushindwa kuzalisha homoni hii na hivyo kupelekea kuongezeka kwiango cha sukari na mwisho kupata ugonjwa wa sukari.


Kuongeza atari ya magonjwa ya moyo na shinikizo la juu la damu


Wanga iliyozidi mwilini na kubadilishwa kuwa mafuta huweza kujikusanya kwenye mishipa ya damu na kupelekea magonjwa ya moyo.


Kuoza meno


Kula wanga kwa wingi kunaongezaatari ya meno kuoza kwani bakteria waliopo mdomoni humeng'enya mabaki ya wanga na kutengeneza tindikali ambayo huozesha meno kwa kusabisha mashimo madogomadogo kwenye meno.Kuepuka hili ni muhimu kuswaki angalau mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni.


Pia kuna tafiti zinazoonesha kua kula vya kula vya wanga pekee na kwa muda mrefu kunapunguza ufanisi wa ufanyaji kazi wa ubongo.


Video inayofuata ina maelezo kuhusu vyakula vya wanga



Imeboreshwa,
6 Aprili 2022, 19:04:30
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Neuro. Why You Should Add Resistant Starch to Your Diet. .https://getneuro.com/blogs/thinktank/why-you-should-add-resistant-starch-to-your-diet. Imechukuliwa 18.04.2020

  2. Encyclopedia britanica.Starch. https://www.britannica.com/science/starch. Imechukuliwa 18.04.2020

  3. Healthline. 19 food that are highin starch. https://www.healthline.com/nutrition/high-starch-foods. Imechukuliwa 18.04.2020

  4.  Starch in food Starch definition . What is starch. https://starchinfood.eu/question/what-is-starch/. Imechukuliwa 18.04.2020

bottom of page