Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, Co
Jumapili, 27 Machi 2022
Zukini
Zukini ni aina ya boga mwitu kutoka kundi la Cucurbita pepo, huvunwa ingali bado changa na kutumika kama chakula baada ya kuchemshwa/kupikwa au kuokwa. Zukini hupendwa kutumiwa na jamii nyingi hiyo ni kutokana na uwepo wa madini na vitamini kwa ajili ya ukuaji wa miili yetu.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Zukini
Mafuta
Madini
Sukari
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Zukini
Zukini ina kemikali muhimu ziitwazo Zeaxanthin na Dehydroascorbic Acid
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100
Nishati = 34kcal
Mafuta = 0.3g
Maji = 88.11g
Kabohaidreti = 7.4g
Sukari = 9.6g
Nyuzilishe = 0.8g
Protini = 1g
Vitamini zinazopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100
Vitamini A = 8mcg
Vitamini B1 = 0.034mg
Vitamini B2 = 0.075mg
Vitamini B3 = 0.355mg
Viatmini B6 = 0.122mg
Vitamini B9 = 17mcg
Vitamini C =12.6mg
Vitamini E =0.10mg
Vitamini K = 3.6mg
Madini yanayopatikana kwenye Zukini lenye gramu 100
Kalishiamu = 15mg
Kopa = 0.04mg
Madini Chuma = 0.31mg
Magineziamu = 15mg
Fosifolasi = 32mg
Potashiamu = 217mg
Sodiamu = 951mg
Zinki = 0.27mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Zukini
Kuimarisha afya macho na kuongeza uwezo kuona na kupunguza magonjwa ya macho yatokanayo na uzee.
Kuimarisha kinga ya mwili
Kupunguza athari ya kupatwa na kansa ya tezi dume na kansa nyingine
Kuimarisha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula
Kusaidia kupunguza uzito usiohitajika mwilini
Kushusha kiwango cha sukari mwilini
Kusaidia kuimarisha na kuboresha afya ya moyo
Kusaidia kuzuia kupatwa na ugonjwa wa rovu
Imeboreshwa,
27 Machi 2022, 17:47:34
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Zucchini. https://www.nutritionvalue.org/Zucchini%2C_pickled_75535000_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.
Wang X, Tanaka M, Peixoto HS, Wink M. Cucurbitacins: elucidation of their interactions with the cytoskeleton. PeerJ. 2017 May 30;5:e3357. doi: 10.7717/peerj.3357. PMID: 28584704; PMCID: PMC5452965. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/28584704/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.
Cha KH, Koo SY, Lee DU. Antiproliferative effects of carotenoids extracted from Chlorella ellipsoidea and Chlorella vulgaris on human colon cancer cells. J Agric Food Chem. 2008 Nov 26;56(22):10521-6. doi: 10.1021/jf802111x. PMID: 18942838. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/18942838/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.
Role of Zucchini and Its Distinctive Components in the Modulation of Degenerative Processes: Genotoxicity, Anti-Genotoxicity, Cytotoxicity and Apoptotic Effects. Written by Damián Martínez-Valdivieso, Rafael Font et al. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5537869/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.