Tango ni zao linalopatikana kwenye familia ya Cucurbitaceae, umbo lake maarufu ni duara ambapo hutumika kama tunda japo pia hutumika kama mboga au kiungo baada ya kuchemshwa.
Taboli ni mchanganyiko wa mboga mboga unaopatikana baada ya kuchanganya nyanya, kitunguu , minti na limao. Hutumika kama kionjo kwenye chakula huku wengine wakifanya kama mlo kamili kwa madhumuni fulani ya kiafya.
Spinachi ni mboga za kijani zitokanazo na mimea ya maua zinazopatikana kwenye familia ya Amaranthaceae. Majani yake hutumika yakiwa mabichi au baada ya kupikwa.