Kufeli sugu kufanya kazi kwa figo (chronic kidney disease)
Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
Hili ni tatizo la kupoteza uwezo wa kufanya kazi kwa figo linalotokea taratibu na kwa uendelevu.Figo hufanya kazi ya kuchuja sumu na kuondoa kiwango cha maji kilichozidi na kuyatoa pamoja na sumu hizo katika mkojo. Kama ugonjwa wako wa figo umefikia hatua mbaya basi kiwango cha maji na sumu zinazotolewa na kiungo hiki hukusanyika katika mwili.
Kwenye hatua za awali za tatizo sugu la figo kufeli kufanya kazi unaweza usipate dalili ashiria ama unaweza kupata dalili chache sana, na unaweza usipate dalili mpaka figo ifikie hatua za mwisho za kufeli
Matibabu ya figo kufeli kufanya kazi huhusisha kuzuia uendelevu wa figo kufeli yaani kutoka hatua moja ya kufeli kwenda nyingine. Na siku zote ni kutibu kitu kinachosababisha figo kufeli kufanya kazi
Kwa sababu tatizo la figo kutofanya kazi linaweza kusababisha ugonjwa figo kufika ukomo wa kufanya kazi ambapo mtu atakufa na hivyo atahitaji kubadilishiwa figo ama kupewa mashine ya kusafisha damu yaani figo bandia
endelea kusoma kwa kubonyeza hapa , Dalili, Visababishi, Vihatarishi, Madhara, Vipimo , Matibabu
ULY CLINIC inakukumbusha siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kwa kubonyeza 'Pata tiba" au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.
Imechapishwa 3/3/2014
imeboreshwa 21/11/20120