Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
​
Fistula kati ya haja kubwa na Uke(Fistula ya Rektovajaino )
​
Utangulizi
​
Fistula ni mawasiliano yanayotoea kati ya kuta za ndani za organi moja na nyingine, hivyo fistula huwa ni tundu linalounganisha organi moja na nyingine kama vile sehemu ya haja kubwa na kibofu au uke, uke na kibofu na kadhalika
Fistula ya Rektovagaino ni ile inayotokea kati ya sehemu ya mwisho ya utumbo mpana na uke. Mazao yoyote yale ya chakula yanayopita katika utumbo mpana yanaweza kupita kwenye fistula na kuingia kwenye uke, kwa maana kwamba gesi au kinyesi.
Fistula aina hii huweza kutokea kutokana na mataizo wakati kujifungua motto, magonjwa ya utumbo mpana kama crohn's, magonjwa yanayosababisha michomo kwenye utumbo mpana, kupigwa mionzi ya x-ray, saratani kwenye maeneo ya nyonga au madhara yatokanayo na matokeo ya upasuaji kwenye maeneo haya ya nyonga.
​
Dalili za fistula kati ya haja kubwa na uke
Dalili za fistula hii mara nyingi husababisha matatizo ya kisaikologia, kujihisi vibaya, kukosa heshima kwa wanawake na wakati mwingine hata kuvunjika kwa mahusiano au ndoa
Fistula ndogo huweza kupona bila matibabu kwa wakti mwingine, na kama haiwezekani basi mwanamke atahitaji matibabu ya upasuaji ili kuziba tundu hili.
Dalili za fistula hii hutegemea na ukubwa wa tundu, mtu anaweza kuwa na dalili chache au dalili mbaya ambapo anashindwa kuzuia kinyesi au kufanya usafi. Mwanamke mwenye fistula anaweza kupata dalili zifuatazo;
​
-
Kupitisha gesi, kinyesi au usaha kwenye tundu la uzazi
-
Harufu mbaya(ya muozo) kutoka ukeni
-
Maambukizi ya mara kwa mara ya ukeni au ya njia ya mkojo
-
Kuwashwa au maumivu kwenye maeneo ya uke na mkundu
-
Maumivu wakati wa kufanya mapenzi au tendo la ndoa
Nini husababisha fistula?
Mambo yafuatayo yanaweza kusababisha fistula hii
-
Majeraha au jeraha wakti wa kujifungua. Majera ukeni wakati wa kujifungua ni njia kuu inayosababisha fistula kwa kiasi kikubwa. Majeraha ya sehemu za uke yanayokaribia kwenye utumbo mpana au mchano wa kuongeza njia na maambukizi wakati wa kujifungua. Mambo haya huweza kutokea kama mwanamke akishikwa na uchungu kwa muda mrefu au kupata uzazi wa shida.fistula inayotokea wakti wa kujifungua huweza kusababisha kulegea kwa misuli inayozuia kinyesi kutoka na hinyo mtu kushindwa kuzua kinyesi na hutoka chenyewe.
-
Ugonjwa wa crohns disease. Aina hii ni ya pili katika kusababisha fistula kaati ya mkundu na uke. Ugojwa huu ni aina ya michomo inayotokea kwenye ukuta wa ndani wa utumbo mpana huungua kutokana na chembe za kupambana na maradhi kuvamia kuta za utumbo. Wanawake wengi wenye ugonjwa huu hawapati fistula aina hii lakini huongeza hatari ya kupata fistula
-
Saratani na matumizi ya mionzi kwenye viungo vya nyonga. Saratani kwenye mkundu au, shingo ya kizazi, tundu la uzazi, mfuko wa kizazi, au mfuko wa kutunzia kinyesi kwa muda (anua canal) huweza kusababisha kutokea kwa fistula. Mionzi inayotumika kama matibabu ya saratani humweka mtu hatarini pia kupata fistula hii kwa sababu mionzi hiyo huua chembe hai za maeneo hayo. Fistula anayotokea kutokana na mionzi hutokea miaka miwili toka mtu alipopata matibabu hayo
-
Upasuaji unaofanya kwenye maeneo haya ya tundu la uzazi, ukuta kati ya uke na mkundu au kimfuko cha kutunzia kinyesi kwa muda. Kufanyiwa upasuaji kama wa kuondolewa kizazi kwa kiasi Fulani huweza kusababisha kupata fistula
Visababishi vingine.kwa kiasi kidogo sana fistula aina hii huweza kutokea kutokana na maambukizi kwenye kuta za tundu la uzazi au mkundu, maambukizi ya utumbo mpana, kutengenezwa kwa vimfuko kwenye utumbo mpana kitaalamu diverticulum, michomo ya muda mrefu kwenye utumbo mpana na mkundu kama kwenye ugonjwa wa ulcerative colitis au majeraha kwenye tundu la uzazi mbali nay ale ya kujifungua.
Madhara ya fistula ya RVF
Madhara yanayoweza kutokana na fistula hii huweza kuwa
​
-
Kushindwa kuzuia kinyesi
-
Matatizo ya usafi maeneo ya uke
-
Maambukizi ya mara kwa mara ya uke na njia ya mkojo (UTI)
-
Miwasho na michomo kwenye uke, ukuta kati ya mkundu na uke au maeneo ya ngozi yanayozunguka mlango wa kinyesi
-
Maambukizi kwenye tundu la fistula huweza kusababisha usaha na huweza kutishia maisha kama tatizo hili lisipotibiwa
-
Kujirudia kutokea kwa fistula
Kumbuka. Kati ya wanawake wanaopata fistula kwa sababu ya ugonjwa wa crohns, hatari ya fistula hii kujirudiani kubwa baada ya matibabu.
​
Vipimo vya fistula
Unaweza kutegemea kupimwa vipimo kadhaa ufikapo hospitali ili kuwezakuambiwa ni tatizo gani linalokusumbua. Vipinmo vifuatavyo vinaweza kufanyika ;
Vipimo vya awali
Dakitrari atapima vipimo vya awali kwa kukuchunguza kabla ya vipimo vingine kuangali kama una saratani, uvimbe wowote ule, maambukizi au mtungo wa usaha. Uchunguzi utafanywa kwenye uke na sehemu za haja kubwa kwa kutumia mkono au vidole vilivyovalishwa glavu
​
Kama fistula ikiwa mbali sana/nyuma sana na sehemu za mbele na uke basi dakitari atatumia kifaa kinachoitwa speculum kitakachomsaidia kupanua uke ili kuona kwa kina-ndani zaidi. Na kifaa kinachofanana na hicho yaani protoscopy kinaweza kutumiwa pia kuangalia maeneo haya na anaweza kuchukua vinyama kwenda kupima maabara akiwa anafanya vipimo
Vipimo vya kugundua fistula
​
Fistula maranyingi huwa haionekani wakati wa vipimo vya awali vya dakitari kutokana na kuwa na tundu dogo sana au mbali na maeneo ya karibu na nnje ya uke, hivyo dakitari ataagiza kufanya vipimno vingine vinavyoweza kusaidia aina ya matibabu unayotakiwa kufanyiwa
Kipimo cha kutumia kemikali kimiminika chenye rangi.
​
Kemikali iitwayo barium enema inawezakusaidia kutambua mahali fistula ilipo na kutofautisha kwamba fistula hii ipo kwenye njia ya haja kubwa nauke au kibofu cha mkojo na uke. Kipimo hiki kikiwa lkinafanyika, picha ya x-ray puia huchukuliwa
kipimo cha kutumia dye ya blue
​
Utawekewa pedi inayoweza kuingia kwenye uke kwa kitaalamu huitwa tampooni, kasha maji haya yenye rangi ya bluu huwekwa kwa sindani sehemu ya haja kubwa. Kama rangi hii ya blue itaonekana kwenye pedi hii basi itajulikana kuwa kunamawasiliano kati ya uke na sehemu ya haja kubwa
​
Vipimo vingine vinavyowe kufanyika ni vya mionzi ya CT na MRI ambavyo vinaweza kuonyesha sehemu hizi kwa undani zaidi,
Kipimo cha mionzi sauti au ultrasound kinaweza kufanyika. Dakitari ataweka kifaa hiki kwenye uke au sehemu ya haja kubwa
Endapo dakitari wako atagundua kwamba unaugonjwa kama wa ulcerative colitis, ataagiza kipimo cha colonoscopy kuangalia utumbo mpana. Wakati wa kufanya kufanya kipimo hiki basi atakata vinyama na kwenda kuvipima maabara kuona kama ugonjwa huu upo
​
​
ULY CLINIC Inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako
​
Wasiliana na datari wa ULY CLINIC kwa ushauri na Tiba kwa kubonyeza Pata Tiba au kupiga namba za simu chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa mara ya mwisho 07.07.2020
​
Rejea za mada hii;
​
-
NCBI. Rectovaginal fistula. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2967329/. Imechukuliwa 07.07.2020
-
Tintinalli's Emergency Medicine: A Comprehensive Study Guide. 8th ed. New York, N.Y.: McGraw-Hill Education. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 07.07.2020
-
Characteristics, management, and outcomes of repair of rectovaginal fistula among 1100 consecutive cases of genital tract fistula in Ethiopia. International Journal of Gynecology & Obstetrics. Imechukuliwa 07.07.2020
-
The role of imaging tests in the evaluation of anal abscesses and fistulas. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 07.07.2020
-
Fecal incontinence. National Digestive Diseases Information Clearinghouse. http://www.niddk.nih.gov/health-information/health-topics/digestive-diseases/fecal-incontinence/Pages/facts.aspx. Imechukuliwa 07.07.2020
-
Toglia MR. Rectovaginal and anovaginal fistulas. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 07.07.2020