Majadiliano na Wataalamu
Vidonge vya kupata hedhi ni vidonge ambavyo ukitumia vitanzisha hedhi. Vidonge hivi huweza kushauriwa na daktari kutumika endapo hedhi imechelewa kwa sababu mbalimbali.
Ufanyaji kazi wa vidonge vya kupata hedhi
Kampaundi za vidonge vya kuanzisha hedhi hufikiriwa kufanya kazi kwa kuathiri moja kwa moja mfumo wa uzazi au kutibu tatizo jingine ambali husababisha kutoingia mwezini.
Orodha ya vidonge vya kuanzisha hedhi
Vifuatavyo ni vidonge vya kupata hedhi;
• Mifepristone
• Misoprostol
Â
Tahadhali ya matumizi ya dawa za kuanzisha hedhi
Dawa hizi zinaweza kusababisha mimba kutoka, na kusababisha utokwe na damu nyingi endapo unatatizo la kutokwa damu, usitumie kabla ya kushauriwa na daktari wako ili kuepuka madhara yoyote yanayoweza kutokea.
Ungependa kufahamu kuhusu dawa za kukata hedhi?
Unaweza kusoma kuhusu vidonge vya kukata hedhi (vidonge vya kuzuia hedhi) kwenye makala nyingine ndani ya tovuti yetu.
Wapi utapata taarifa zaidi kuhusu vidonge vya kupata hedhi?
Wasiliana na daktari wako endapo unahitaji maelezo zaidi kuhusu dawa ya kuanzisha hedhi. Pia unaweza kuuliza maswali kwa daktari wa ULY CLINIC kwa huduma za ushauri na tiba mtandaoni katika linki chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii
1. Drugbank. Menstruation-Inducing Agents. https://go.drugbank.com/categories/DBCAT001155. Imechukuliwa 16.11.2025
2. Springer nature. Menstruation induction. https://link.springer.com/chapter/10.1007/978-1-4471-1931-9_7. Imechukuliwa 16.11.2025
3. Xiao B, et al. Menstrual induction with mifepristone and misoprostol. Contraception. 2003 Dec;68(6):489-94. doi: 10.1016/j.contraception.2003.09.009. PMID: 14698080.
Like