Kwanini homa hutokea baada ya chanjo?
Chanjo hutayarisha mfumo wa kinga ya mwili kuulinda mwili dhidi ya virusi au bakteria wanaoweza kuleta ugonjwa. Homa hii hutokea kwa sababu chanjo huwa na viunda vya vijidudu hivyo ambavyo vinajulikana kuamsha mwitikio wa kinga ya mwili. Hata hivyo, chanjo huwa hazisababishi mwitikio wa unaoweza kumfanya mtu kuugua ugonjwa kama wanavyosababisha vimelea asili. Kwa baadhi ya watu, mwitikio wa kinga ya mwili huwa na nguvu ya kutosha kusababisha dalili zinazoweza kuonekana kama vile homa kali.
Nini unapaswa kufanya unapopata homa?
Mara nyingi si lazima kutumia dawa za kushusha homa kama vile paracetamol unapopatwa na homa baada ya kuchoma chanjo. Inashauriwa kunywa maji ya kutosha tu wakati huu. Kama unafikiria homa ni kali au inakupelekea kukulaza, wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba.
Rejea za mada hii:
Ahn SH, Zhiang J, Kim H, Chang S, Shin J, Kim M, Lee Y, Lee JH, Park YR. Postvaccination Fever Response Rates in Children Derived Using the Fever Coach Mobile App: A Retrospective Observational Study. JMIR Mhealth Uhealth. 2019 Apr 22;7(4):e12223. doi: 10.2196/12223. Erratum in: JMIR Mhealth Uhealth. 2020 May 7;8(5):e18921. PMID: 31008712; PMCID: PMC6658305.
Childrens hospital of philadelphia. Fever and Vaccines. https://www.chop.edu/centers-programs/vaccine-education-center/vaccine-safety/fever-and-vaccines. Imechukuliwa 16.07.2022
Kaiser permanent. Immunization that causes fever. https://healthy.kaiserpermanente.org/health-wellness/health-encyclopedia/he.immunizations-that-may-cause-fever.not35603/. Imechukuliwa 16.07.2022
Settle childrens.Immunization Reactions.https://www.seattlechildrens.org/conditions/a-z/immunization-reactions/#:. Imechukuliwa 16.07.2022