Magonjwa ya ngono hufahamika pia kama magonjwa ya zinaa, ni magonjwa yanayoenezwa kwa njia ya kujamiana. Kuna njia mbalimbali za kujamiana ambazo zinafahamika. Njia zote hizi zinaweza kuwa chanzo cha kueneza magonjwa hayo.
Makundi ya maonjwa ya ngono
Magonjwa ya ngono yamegawanywa kwenye makundi mawili makuu, magonjwa ya ngono yanayotibika na yale yasiyotibika. Mifano ya magonjwa hayo imeelezewa hapa chini, kusoma zaidi bofya ugonjwa husika.
Magonjwa ya ngono yanayotibika
Baadhi ya magonjwa ya ngono yanayotibika ni:
Klamidia (Chlamydia)
Chawa wa mavuzi
Maikoplazma genitalium
Granuloma inguinale
Skebiz (Scabies)
Chankroidi (chankroid)
Limfagranuloma veneramu (LVG)
Magonjwa ya zinaa yasiyotibika
BAadhi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibika kwa sasa ni:
Virusi vya herpes aina ya 1 na 2 (virusi vya malenge aina 1 na 2)
Kirusi cha human papilloma (HIV)
Namna ya kujikinga na magonjwa ya ngono
Mambo yafuatayo yanaweza kukukinga kupata magonjwa ya ngono.
Kuacha ngono
Njia pekee na madhubuti ya kukinga maambukizi ya magonjwa ya zinaa ni kuacha kushiriki ngono aina yoyote ile
Tumia kondomu
Endapo unashindwa kuacha kushiriki ngono, unaweza tumia kondomu kwa namna sahihi ili kuepuka magojwa ya zinaa. Kumbuka unaweza kupata magonjwa endapo kondom itapasuka au endapo utashiriki ngono ya kuhusisha midomo kwa mdomo, au uke kwa uke, njia ambazo ni vigumu kutumia kondomu.
Punguza idadi ya wapenzi unaofanya nao ngono
Kupunguza idadi ya wapenzi unaoshiriki nao ngono itapunguza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa. Ni vema wewe na mpenzi wako mkapima na kushirikishana majibu endapo mmekaa muda mrefu bila kukutana kwa usalama wenu.
Pata chanjo
Kupata chanjo ya zinazopatikana kama ya HPV, HBV na zingine zinapunguza hatari ya kupata magonjwa ya zinaa ambayo hayana tiba. Licha ya kupata chanjo bado utahitajika kujikinga na hatari za kupata maambukizi kwa njia zingine zilizotajwa hapo juu.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?
Wasiliana na daktari wako siku zote kwa maelezo zaidi na tiba.
Soma zaidi makala hii katika mada ya magonjwa ya zinaa
Rejea za mada hii:
1. NHS. STIs. https://www.nhs.uk/conditions/sexually-transmitted-infections-stis/. Imechukuliwa 02.07.2021 2. CDC. Sexually transmitted diseases.https://www.cdc.gov/std/general/default.htm. Imechukuliwa 02.07.2021 3. CDC. STDs treatment. https://www.cdc.gov/std/treatment/default.htm. Imechukuliwa 02.07.2021 4. WHO. STIs. https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/sexually-transmitted-infections-(stis). Imechukuliwa 02.07.2021 5. Michael Ray Garcia, et al. Sexually Transmitted Infections. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK560808/. Imechukuliwa 02.07.2021 6. Treatments for Lymphogranuloma Venereum (LGV). https://stanfordhealthcare.org/medical-conditions/sexual-and-reproductive-health/lgv/treatments.html#. Imechukuliwa 02.07.2021 7. Ye X, et al. Trends in the Epidemiology of Sexually Transmitted Disease, Acquired Immune Deficiency Syndrome (AIDS), Gonorrhea, and Syphilis, in the 31 Provinces of Mainland China. Med Sci Monit. 2019 Jul 30;25:5657-5665. [PMC free article] [PubMed] 8. De Schryver A, et al. Epidemiology of sexually transmitted diseases: the global picture. Bull World Health Organ. 1990;68(5):639-54. 9. Featherston WE. Sexual identity and practices relating to the spread of sexually transmitted diseases. Prim Care. 1990 Mar;17(1):29-45. 10. Capriotti T. HIV/AIDS: An Update for Home Healthcare Clinicians. Home Healthc Now. 2018 Nov/Dec;36(6):348-355. 11. Ghanem KG, et al. Screening for sexually transmitted infections. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 02.07.2021 12. U.S. Centers for Disease Control and Prevention. Screening recommendations and considerations referenced in the 2015 STD treatment guidelines and original sources. https://www.cdc.gov/std/tg2015/screening-recommendations.htm. Imechukuliwa 02.07.2021