Kunywa maji mengi kupitiliza
Haishauriwi kiafya kunywa maji mengi zaidi ya mahitaji ya mwili wako kwa kuwa kiwango kinachozidi huweza geuka kuwa sumu. Kwa bahati mbaya dalili za sumu ya maji kutokana na kunywa maji mengi huwa ngumu kutambuliwa kirahisi na wataalamu wa afya kwa kuwa dalili zake hufanana na magonjwa ya akili, endapo tatizo lisipofahamika mapema na kupata tiba huleta madhara makubwa pamoja na kifo.
Tatizo la sumu ya maji linalotokea kutokana kuwa na maji mengi mwilini kuliko kiwango cha chumvi hutokea kwa nadra na huweza pelekea kifo.
Dalili za mtu aliyekunywa maji mengi kupitiliza
Utambuzi wa mtu aliyeathirika na maji huwa si rahisi kutokana na dalili zake kuhusiana na matatizo mengine yanayoweza kufikiriwa kuwa ugonjwa wa akili.
Kama mtu akinywa maji mengi kupitiliza kwa haraka anaweza kupata dalili za awali zifuatazo;
Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya kichwa
Kuchanganyikiwa au kuchanganya mambo
Maumivu ya kubana kwa misuli
Kukojoa mara kwa mara
Kuvimba mwili, miguu mikono na tumbo
Dalili za baadae za kunywa maji mengi kupita kiasi
Dalili za baadae zinazoashiria tatizo kuwa kubwa zaidi huwa pamoja na:
Kupata hisia ya kutopendwe au kukubalika
Kupata hisia zisizo halisi na imani potofu
Kuona vitu visivyoonekana na watu wengine
Kusikia sauti zisizosikiwa na watu wengine
Kuchanganyikiwa( Kukanganya mambo)
Kupoteza fahamu
Kutambulika huwa muhimu ili kuzuia dalili zingine za degedege na kuzimia. Tatizo lisipogundulika linaweza kupelekea kifo.
Visababishi vya kunywa maji mengi kupita kiasi
Licha ya tatizo kutokea kwa nadra sana, sumu ya maji inaweza kusababishwa na sababu mbalimbali ambazo ni;
Mazoezi: kunywa maji mengi baada ya mazoezi ya muda mrefu pasipo kurejesha madini yaliyopotea kwenye jasho
Kunywa maji mengi kutokana na matatizo ya kisaikolojia ya kupata kiu kupitiliza
Kunywa maji ya kutosha kama adhabu au kwenye mashindano
Kuishiwa maji kwenye hali ya kuwa na kiwango kikubwa cha homoni (ADH)
Kufanya kazi kwenye hali ya hewa ya joto
Matumizi ya dawa kama dawa zinazoongeza kiu kama vile dawa za magonjwa ya akili au usumu wa dawa jamii ya NSAIDS na dawa za kupunguza maji mwilini
Magonjwa ya figo yanayopelekea kutochunjwa vema kwa maji
Ugonjwa wa ini na Schizophrenia
Kuferi kwa moyo
Mambo ya kufanya ili usizidishe kiwango cha maji
Kunywa maji kulingana na kiu unayopata na hali yako ya kiafya, usinywe zaidi ya lita moja kwa saa au kujilazimisha
Chunguza rangi ya mkojo unayopata wakati wa kukojoa, mkojo unapaswa kuwa wa njano mpauko. Kama una rangi ya maji inaweza kuonyesha umekunywa maji mengi hivyo usiendelee mpaka utakapopata kiu.
Acha kunywa maji kama unajisikia kichefucehfu na kutapika au maumivu ya kichwa- dalili hizi ni dalili za awali za kuwa na maji mengi mwilini.
Acha kunywa maji endapo kiu imekata
Jifunze kuusikiliza mwili wako unataka maji au la.
Madhara ya kunywa maji mengi kupita kiasi
Degedege
Kupoteza fahamu
Kifo
Rejea za mada hii:
Lee LC, Noet al. When Plenty Is Too Much: Water Intoxication in a Patient with a Simple Urinary TractI nfection (https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5129180/). BMJ Case Rep. 2016 Nov 1;2016:bcr2016216882. Imechukuliwa 29.10.2024
Merck Manual Consumer Version. Overhydration (https://www.merckmanuals.com/home/hormonal-and-metabolic-disorders/water-balance/overhydration). Last reviewed 5/2024. Imechukuliwa 29.10.2024
Peechakara BV, e tal. Water Toxicity (https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK537231/). 2023 Jun 26. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island, FL: StatPearls Publishing; 2024 Jan. Imechukuliwa 29.10.2024
Renal Function & Micturition. In: Barrett KE, et al, eds. Ganong’s Review of Medical Physiology. 26th ed. McGraw-Hill Education; 2019.
Siegel AJ. Fatal water intoxication and cardiac arrest in runners during marathons: prevention and treatment based on validated clinical paradigms. Am J Med. 2015 Oct;128(10):1070-5.
Umansky L, Sella A. [Psychogenic polydipsia leading to water intoxication]. Harefuah. 2000 Jan 02;138(1):9-12, 87.
Water intoxication. https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/water-intoxication. Imechukuliwa 29.10.2024