
Majimaji ya ukeni ni sehemu muhimu ya mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo husaidia kulinda uke dhidi ya maambukizi, kuweka unyevunyevu, na kusaidia katika uzazi. Rangi, muundo, na kiasi cha majimaji haya hubadilika kulingana na mzunguko wa hedhi, hali ya kiafya, au maambukizi.
Kuna aina 7 za majimaji ukeni ambazo zimeelezewa katika makala hii kiundani pamoja na maana yake katika tiba.
Majimaji safi yanayovutika (yenye utelezi)
Kupata majimaji safi yanayovutika ni hali ya kawaida inayotokea wakati wa uovuleshaji.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Kupata majimaji safi yenye utelezi huwa ishara nzuri ya wakati wa kutafuta ujauzito na humaanisha kuwa yai limepevuka na mwili uko tayari kunasa ujauzito.
Majimaji meupe yasiyo na utelezi
Majimaji meupe yasiyo na utelezi huonekana wakati wa kuushughulisha mwili na wakati wa ngono.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Kupata majimaji haya ni sehemu ya afya ya uke na haionyeshi tatizo lolote.
Majimaji meupe mithiri ya maziwa mgando
Kuupata majmaji meupe mazito mithiri ya maziwa mgando ni jambo la kawaida mwanzoni au mwishoni mwa hedhi.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Ikiwa unapata majimaji haya na yanaambatana na kuwasha na harufu mbaya, yanaweza kuashiria maambukizi ya fangasi ukeni na hivyo utahitaji tiba.
Majimaji ya njano au kijani
Majimaji ya njano au kijani si ya kawaida katika uke na mara nyingi huashiria maambukizi.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Ikiwa majimaji haya ya njano au kijani ni mazito na yana harufu mbaya, yanaweza kuwa ishara ya magonjwa ya zinaa kama Trikomoniasis au klamidia.
Majimaji ya kijivu yenye harufu ya samaki
Kutokwa majimaji ya kijivu yenye harufu ya samaki ni dalili ya maambukizi ya bakteria kwenye ukeni.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Kutokwa majimaji ya kijivu yenye harufu ya samaki inaashiria ugonjwa wa Bacterial Vaginosis, ambao unahitaji matibabu ya kutumia dawa jamii ya antibiotiki.
Majimaji ya kahawia au mekundu
Kupata majimaji ya kahawia au mekundu huashiria damu iliyochanganyika na majimaji ya uke.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Ikiwa majimaji ya kahawia au mekundu yatatokea kati ya mizunguko ya hedhi, inaweza kuwa ishara ya mabadiliko ya homoni, ujauzito wa nje ya kizazi, au matatizo ya uzazi kama saratani ya kizazi.
Majimaji mepesi ya njano
Kupata majimaji mepesi ya njano yasiyo na harufu mbaya, inaweza kuwa hali ya kawaida.
Umuhimu wa majimaji haya katika tiba
Ikiwa majimaji mepesi ya njano yanaambatana na harufu kali na muwasho, yanaweza kuashiria maambukizi ya bakteria au magonjwa ya zinaa.
Wakati gani wa kuwasiliana na daktari unapotokwa na ute usio wa kawaida ukeni?
Unapaswa kumuona daktari ikiwa endapo unapata majimaji na hali zifuatazo
Kupata majimaji yenye harufu kali isiyo ya kawaida
Kupata majimaji yenye rangi isiyo ya kawaida kama kijani au kijivu
Kupata majimaji yanayoambatana na maumivu ya tumbo au uke
Kupata majimaji yanayoambatana na muwasho mkali au upele ukeni
Kupata majimaji yanayoambatana na maumivu wakati wa kukojoa
Rejea za mada hii:
Brunham RC, et al. Mucopurulent cervicitis—the ignored counterpart in women of urethritis in men. N Engl J Med. 1984;311:1–6.
Eschenbach DA. Vulvovaginal discharge. In: Peckham BM, Shario SS, eds. Signs and symptoms in gynecology. Philadelphia: JB Lippincott, 1983;254–61.
Fleury FJ. Adult vaginitis. Clin Obstet Gynecol. 1981;24:407–38.
Hill LV,  et al. Vaginitis. Current microbiologic and clinical concepts. Can Med Assoc J. 1986;134:321–31.
*Holmes KK. Lower genital tract infections in women: cystitis/urethritis, vulvovaginitis, and cervicitis. In: Holmes KK, Mardh PA, Sparling PF, et al., eds. Sexually transmitted diseases. New York: McGraw-Hill, 1984;557–89.
Sobel JD. Bacterial vaginosis—an ecologic mystery. Ann Intern Med. 1989;111:551–52.
Spence MR, et al. The clinical and laboratory diagnosis of Trichomonas vaginalis infection. Sex Transm Dis. 1980;7:168–71.
KRANTZ KE. The gross and microscopic anatomy of the human vagina. Ann N Y Acad Sci. 1959 Nov 18;83:89-104.
WELLS LJ. Embryology and anatomy of the vagina. Ann N Y Acad Sci. 1959 Nov 18;83:80-8.
Paavonen J. Physiology and ecology of the vagina. Scand J Infect Dis Suppl. 1983;40:31-5.
Anderson DJ, et al. The structure of the human vaginal stratum corneum and its role in immune defense. Am J Reprod Immunol. 2014 Jun;71(6):618-23.
Forsberg JG. Estrogen, vaginal cancer, and vaginal development. Am J Obstet Gynecol. 1972 May 01;113(1):83-7.
Levin RJ. Sexual arousal--its physiological roles in human reproduction. Annu Rev Sex Res. 2005;16:154-89.
Dawson SJ, Sawatsky ML, Lalumière ML. Assessment of Introital Lubrication. Arch Sex Behav. 2015 Aug;44(6):1527-35.
Chambliss KL, et al. Estrogen modulation of endothelial nitric oxide synthase. Endocr Rev. 2002 Oct;23(5):665-86.