Bronkaitiz hutokana na michomo ya kinga za mwili kwenye njia ya hewa inayoamushwa na maambukizi ya virusi, mara nyingi hujitokeza baada ya kuugua mafua. Ugonjwa huu uweza kuisha wenyewe ndani ya siku 10 bila tiba. Wagonjwa wa bronkaitizi mara nyingi hukohoa makohozi mazito yanayoweza kuwa na rangi.
8
2
Daliliza bronkaitiz
Kikohozi kikavu au chenye makohozi ya njano,au kijani katika siku mbili au tatu
Kupumua kwa shida
Kifua kutoa mlio wa filimbi
Homa
Maumivu wakati wa kumeza
Kukauka kwa koo
Kutetemeka
Kuishiwa pumzi
Maumivu ya mwili
Wakati gani wa kumpigia daktari?
Kama dalili ya kikohozi na kupiga miruzi zikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili
Makohozi yanatoka na damu, kujihisi uchovu homa endelevu na kuishiwa pumzi
Kushindwa kulala kwa sababu ya kukohoa
Kupanda kwa joto la mwili
Vihatarishi
Kuvuta sigara-
Kinga ya chini ya mwili – haswa kwa watoto, watu wazima na wanaotumia dawa za kushusha kinga ya mwili
Kujianika kwenye vichokoza mapafu- kemikali za viwandani
Kucheua tindikali
Matibabu
Mara nyingi matibabu ya dawa kwa mtu mwenye afya nzuri si muhimu kwa sababu mwili unakinga ya kutosha kufanya ugonjwa huu kuisha wenyewe.
Endapo dawa zitahitajika zinahusisha;
Dawa ya kulainisha makohozi
Dawa ya kuzuia maumivu kama paracetamol, Diclopar na aspirin(isitumiwe na watoto)
Dawa za kuzuia kikohozi kama Codeine, Dextromethopan au Pholcodeine (Dawa hizi hutumika kuzuia kikohozi kikavu chenye kero kwa mgonjwa. Hivyo zisitumike kwa tiba ya kikohozi laini kwa sababu husababisha makohozi yenye vimelea vya maradhi kubakia kwenye njia ya hewa na hii ni hatari kwa wagonjwa wenye bronkiti sugu)
Matibabu ya nyumbani
Kunywa maji ya kutosha na epuka vitu vyenye pombe au kafeini
Pumzika vya kutosha ili uupatie mwili nafasi ya kujiponya
Ongeza unyevu kwenye hewa unayovuta au kwa kujifukiza
Madhara ya bronchaitiz kali
Mgonjwa mwenye Bronkiti kali anaweza kupata ambukizo la ziada kutokana na bakteria hivyo kupata nimonia ambapo dalili ya homa itaongezeka. Hii italazimu kutibiwa kwa kutumia dawa sahihi za kuua vimelea husika vya bakteria. Onana na daktari endapo una kikohozi pamoja na homa kwa ushauri na tiba
Kinga
Acha kuvuta sigara
Nawa mikono haswa kama kinga ya mwili iko chini
Pacha chanjo ya kirusi cha Influenza
Vaa barakoa maalumu ya kukukinga na sumu katika hew kama unafanya kazi viwandani kwenye gesi kali zinazochokoza koo
Rejea za mada hii;
CDC. Acute bronchitis. https://www.cdc.gov/antibiotic-use/bronchitis.html. Imechukuliwa
National Heart, Lung, and Blood Institute. What is bronchitis?. http://www.nhlbi.nih.gov/health/health-topics/topics/brnchi. Imechukuliwa 20.07.2021
Goldman L, et al. Acute bronchitis and tracheitis. Goldman's Cecil Medicine. 25th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. http://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 20.07.2021
Stoller JK, et al. Management of infection in acute exacerbations of chronic obstructive pulmonary disease. http://www.uptodate.com/home. Imechukuliwa 20.07.2021
Tintinalli's Emergency Medicine. Tintinalli JE, et al. Acute bronchitis and upper respiratory tract infections. A Comprehensive Study Guide. 8th ed. New York, N.Y.: The McGraw Hill Companies; 2016. http://accessmedicine.com. Imechukuliwa 20.07.2021
Acute bronchitis. American Lung Association. http://www.lung.org/lung-health-and-diseases/lung-disease-lookup/acute-bronchitis/learn-about-acute-bronchitis.html. Imechukuliwa 20.07.2021
Gautret P, et al. Travel-associated illness in older adults (>60 y). Journal of Travel Medicine. 2012;19:169.
Centers for Disease Control and Prevention. Antibiotics aren't always the answer. https://www.cdc.gov/features/getsmart/. Imechukuliwa 20.07.2021
Harris AM, et al. Appropriate antibiotic use for acute respiratory tract infection in adults: Advice for high-value care from the American College of Physicians and the Centers for Disease Control and Prevention. Annals of Internal Medicine. 201;164:425.
Environmental Protection Agency. Use and care of home humidifiers. https://www.epa.gov/indoor-air-quality-iaq/indoor-air-facts-no-8-use-and-care-home-humidifiers. Imechukuliwa 20.07.2021