Je chanjo ya rota kwa mtoto wa miez sita husababisha homa kwa mtoto?
NDIO!
Homa ni mojawapo ya maudhi ya kawaida ya chanjo. Kwa kuwa mara nyingi homa huhusishwa na ugonjwa, wazazi wengi hupata wasiwasi wakati mtoto akipaya homa baada ya chanjo. Hata hivyo ni vema mzazi kufahamu kuwa, homa wakati huu ni kawaida kutokea na huashiria mwitikio wa kinga ya mwili dhidi ya chanjo.
Kwanini homa hutokea?
Chanjo hutayarisha mfumo wa kinga ili kulinda mwili dhidi ya virusi au bakteria wanaoweza kuleta ugonjwa. Homa hii hutokea kwa sababu chanjo huwa na viunda vya vijidudu hivyo ambavyo vinajulikana kuamsha mwitikio wa kinga. Hata hivyo, chanjo hazitasababisha mwitikio wa kutosha wa kinga ya mwili ambao unaweza kumfanya mtu kuugua ugonjwa kama wanavyosababisha vimelea asili. Hata hivyo kwa baadhi ya watu mwitikio wa kinga ya mwili huwa na nguvu ya kutosha kusababisha dalili zinazoweza kuonekana kama vile homa kali.
Homa hutokea baada ya muda gani?
Mara nyingi homa hutokea ndani ya siku 7 baada ya kuchoma chanjo
Ufanyaje mtoto anapopata homa?
Mara nyingi dawa za kushusha homa huwa hazihitajiki isipokuwa kama mtoto amepata homa kali au kuonekana amelegea. Mambo unayoweza kufanya kama hujampa dawa ya kushusha homa ni mosi, kuhakikisha kuwa anapata maji ya kutosha(kutoka kwenye vyakula n.k), kama ananyonya tu, hakikisha ananyonya vya kutosha, pili kama unadhani mtoto anahitaji kupata dawa ya kushusha homa, wasiliana na daktari kwa ushauri kabla ya kufaya hivyo.
Rejea za mada hii:
Ahn SH, Zhiang J, Kim H, Chang S, Shin J, Kim M, Lee Y, Lee JH, Park YR. Postvaccination Fever Response Rates in Children Derived Using the Fever Coach Mobile App: A Retrospective Observational Study. JMIR Mhealth Uhealth. 2019 Apr 22;7(4):e12223. doi: 10.2196/12223. Erratum in: JMIR Mhealth Uhealth. 2020 May 7;8(5):e18921. PMID: 31008712; PMCID: PMC6658305.
Childrens hospital of philadelphia. Fever and Vaccines. https://www.chop.edu/centers-programs/vaccine-education-center/vaccine-safety/fever-and-vaccines. Imechukuliwa 16.07.2022
Kaiser permanent. Immunization that causes fever. https://healthy.kaiserpermanente.org/health-wellness/health-encyclopedia/he.immunizations-that-may-cause-fever.not35603/. Imechukuliwa 16.07.2022
Settle childrens.Immunization Reactions.https://www.seattlechildrens.org/conditions/a-z/immunization-reactions/#:. Imechukuliwa 16.07.2022
Can we just be real for a moment looks mean the world. I must pressure this as much as possible! In the web based dating world you don't get another opportunity to establish a decent first connection. The principal thing a lady sees when she's online is your image. That implies you want to tips dating put your best face forward. Try not to get old photographs with you and your young m or you and your ex and post them on the web.