
Amoeba au amoebiasis ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea Entamoeba histolytica. Maambukizi haya mara nyingi huathiri mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hasa utumbo mpana.
Dalili za Amoeba
Dalili za amoeba zimegawanyika katika makundi mbalimbali zikiwa zinaashiria hatua ya ugonjwa, ambapo zinaweza kuwa nyepesi, za wastani, au kali, kulingana na kiwango cha maambukizi.
Dalili nyepesi za amoeba (katika tumbo)
Kuhara kunakoweza kuambatana na kuhara damu au ute
Maumivu ya tumbo
Tumbo kujaa gesi
Kuhisi kichefuchefu
Kupoteza hamu ya kula
Kupungua uzito bila sababu ya msingi
Homa nyepesi
Dalili kali za amoeba wa tumbo (katika tumbo)
Kuhara damu mara kwa mara
Maumivu makali ya tumbo
Homa kali
Uchovu mkubwa kutokana
Upotevu wa maji mwilini
Dalili za amoeba katika Ini
Amoeba akisambaa kwenye ini husababisha ini kutunga usaha, dalili zake ni pamoja na;
Homa kali inayoambatana na jasho
Maumivu makali upande wa juu kulia mwa tumbo (eneo la ini)
Kupungua uzito haraka
Kuhisi uchovu
Kudhoofika mwili
Wakati gani wa kumwona daktari haraka unapokuwa na dalili za amoeba?
Unapaswa kutafuta matibabu ya haraka ikiwa unakumbwa na dalili kali za amoeba kama vile;
Dalili za Upungufu Mkubwa wa maji mwilini
Mfano wa dalili ni kama
Kuhara mfululizo (zaidi ya mara 6 kwa siku)
Kutapika kupita kiasi, kiasi cha kushindwa kunywa maji
Kiu kali, mdomo mkavu, macho yaliyodidimia
Kizunguzungu, kuchanganyikiwa, au kuzimia
Unapata kinyesi chenye damu au maumivu makali ya tumbo
Dalili hii inaweza kuambatana pia na;
Kuhara damu au kinyesi chenye ute mwingi
Maumivu makali ya tumbo au tumbo kuwa na ugumu
Tumbo kuvimba au kuhisi limejaa sana
Unapata dalili za maambukizi ya Ini
Dalili hizo ni kama vile;
Maumivu makali upande wa juu kulia wa tumbo
Homa kali (zaidi ya 38.5°C au 101°F)
Kupungua uzito kwa kasi na uchovu mwingi
Njano kwenye ngozi na macho
Unapata dalili za maambukizi yanayoenea kwenye mwili
Dalili hizo ni kama vile;
Homa kali inayoambatana na kutetemeka na jasho
Kupumua kwa shida au maumivu ya kifua (ikiathiri mapafu)
Tumbo kuvimba na maumivu makali (hatari ya ini kupasuka)
Una dalili za kawaida lakini upo kwenye makundi maalumu
Makundi yaliyo katika hatari zaidi ni kama;
Wajawazito
Watoto wachanga na wadogo
Wazee
Watu wenye kinga dhaifu (wenye HIV, kisukari, saratani, n.k.)
Vipimo vya ugonjwa wa amoeba
Ili kuthibitisha maambukizi ya Entamoeba histolytica (amoeba), madaktari hutumia mchanganyiko wa dalili za mgonjwa, vipimo vya maabara, na historia ya mgonjwa.
Historia ya Mgonjwa na dalili za kitiba
Kuhara kinyesi chenye damu au ute
Maumivu ya tumbo (hasa eneo la chini la tumbo au upande wa kulia juu ikiwa ini limeathirika)
Homa na uchovu ikiwa maambukizi ni makali
Kupungua uzito bila sababu ya msingi
Kichefuchefu au kutapika
Vipimo vya Maabara kwa uchunguzi wa Kinyesi
Hadubini ya wet mount– Kuangalia vimelea vya Entamoeba histolytica chini ya darubini
Kipimo cha antijen kwenye kinyesi(EIA/ELISA) – Kugundua protini za amoeba kwa usahihi zaidi
Kipimo PCR – Hutumika kutofautisha E. histolytica na aina zisizo hatari kama E. dispar
Vipimo vya Maabara kwa uchunguzi wa damu
Kipimo ELISA – Hutambua kingamwili dhidi ya E. histolytica, hasa kwa maambukizi ya muda mrefu
Indirect hemagglutination test (IHA) – Hutumika kwa maambukizi sugu
Vipimo vya picha
Ikiwa kuna dalili za maambukizi katika ini (amoebic liver abscess), vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika:
Ultrasound ya tumbo – Kugundua usaha kwenye ini
CT Scan / MRI – Kuangalia uvimbe au vidonda kwenye ini
Vipimo vya jumla
Vipimo hivi hufanyika ili kuangalia hali ya mwili na kusaidia katika maamuzi ya tiba;
Full Blood Count (FBC) – Inaweza kuonyesha ongezeko la seli nyeupe za damu (leukosaitosis) ikiwa kuna jipu la amoeba
Liver function tests (LFTs) – Ikiwa ini limeathirika, vipimo vya ini vinaweza kuonyesha mabadiliko katika vimeng'enya vya ini na utendaji kazi wake.
Vigezo vya uhakika wa ugonjwa wa Amoeba
Vigezo vifuatavyo vikiwepo, utathibitika kuwa una ugonjwa wa amoeba;
Kimelea Entamoeba histolytica ameonekana katika kinyesi au kinyongo
Dalili na historia inaendana na maambukizi ya amoeba
Ushahidi wa jipu la amoeba kwenye ini kwa kipimo cha Ct scan au ultrasound
Ongezeko la kingamwili dhidi ya kimelea wa amoeba katika vipimo vya damu
Matibabu ya Amoeba
Madaktari hutibu amoeba kwa kutumia dawa kama:
Metronidazole au Tinidazole – Kuua vimelea vya amoeba
Paromomycin – Kuondoa mabaki ya vimelea kwenye utumbo
Dawa za kutibu dalili – Kama vile ORS kwa kuzuia upungufu wa maji mwilini
Jinsi ya Kujikinga na Maambukizi ya Amoeba
Kunywa maji safi na salama
Kuosha matunda na mboga vizuri
Kunawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka chooni
Epuka kula chakula cha mitaani ambacho si safi
Kama una dalili zinazodumu kwa muda mrefu au zinaongezeka, ni muhimu kutafuta matibabu haraka.
Rejea za mada hii;
Saidin S, et al. Update on laboratory diagnosis of amoebiasis. Eur J Clin Microbiol Infect Dis. 2019 Jan;38(1):15-38.
Kumanan T, et al. Amoebic Liver Abscess and Indigenous Alcoholic Beverages in the Tropics. J Trop Med. 2018;2018:6901751.
Shirley DT, et al Review of the Global Burden, New Diagnostics, and Current Therapeutics for Amebiasis. Open Forum Infect Dis. 2018 Jul;5(7):ofy161.
Fleming R, et al. Clinical manifestations and endoscopic findings of amebic colitis in a United States-Mexico border city: a case series. BMC Res Notes. 2015 Dec 14;8:781.
Guevara Á, et al. Use of Real-Time Polymerase Chain Reaction to Differentiate between Pathogenic Entamoeba histolytica and the Nonpathogenic Entamoeba dispar in Ecuador. Am J Trop Med Hyg. 2019 Jan;100(1):81-82.
Chacín-Bonilla L. [An update on amebiasis]. Rev Med Chil. 2013 May;141(5):609-15.
González-Alcaide G, et al. Areas of research and clinical approaches to the study of liver abscess. World J Gastroenterol. 2017 Jan 14;23(2):357-365.
Burchard GD. [Treatment of diseases acquired abroad]. Internist (Berl). 2014 Sep;55(9):1100, 1012.
Anwar A, et al. Combating Acanthamoeba spp. cysts: what are the options? Parasit Vectors. 2018 Jan 09;11(1):26.