Epidemiolojia ya Gono Barani Afrika
Gono ni mojawapo ya magonjwa ya zinaa yanayoenea kwa kasi barani Afrika. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa Afrika ina kiwango cha juu cha maambukizi kutokana na changamoto kama ukosefu wa uelewa wa afya ya ngono, vikwazo vya kupata huduma za afya, na upinzani wa vimelea vya kisonono dhidi ya dawa za antibiotiki Katika baadhi ya nchi, asilimia 3-10 ya wanaume na wanawake wenye magonjwa ya zinaa wanakutwa na gono.
Epidemiolojia ya gono Nchini Tanzania
Gono au kisonono ni miongoni mwa magonjwa ya zinaa yanayoathiri watu wengi duniani, ikiwemo Tanzania. Uchunguzi umeonyesha kuwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwemo gono, ni ya juu miongoni mwa watu wazima katika maeneo ya mijini nchini Tanzania.
Hata hivyo, upatikanaji wa takwimu sahihi kuhusu kiwango cha maambukizi ya gono nchini ni changamoto kutokana na ukosefu wa mbinu bora za uchunguzi na huduma duni za afya.
Dalili za gonokwa Wanaume
Wanaume wengi wenye gono huonyesha dalili ndani ya siku 2 hadi 14 baada ya kuambukizwa. Dalili hizi zinaweza kujumuisha:
Kutokwa na usaha kwenye uume (unaweza kuwa wa rangi ya njano, kijani au nyeupe).
Maumivu au hisia ya kuungua wakati wa kukojoa.
Kuvimba na maumivu kwenye korodani ikiwa maambukizi yameenea
Kukojoa mara kwa mara au kuhisi haja ya kukojoa hata kama kibofu hakijajaa.
Maambukizi kwenye puru (njia ya haja kubwa) yanaweza kusababisha maumivu ya haja kubwa, kutokwa na damu, au usaha.
Maambukizi ya koo yanaweza kutokea kutokana na ngono ya mdomo, ingawa mara nyingi hayana dalili.
Ikiwa gono hakitatibiwa, inaweza kusababisha madhara makubwa kama ugumba, kuenea kwa maambukizi kwenye damu, na matatizo ya viungo.
Kinga ya maambukizi ya gono kwa wanaume
Kwa kuzingatia hatua hizi, inawezekana kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya maambukizi ya Gono na magonjwa mengine ya zinaa. Kujikinga na gono kunajumuisha hatua zifuatazo:
Matumizi sahihi ya kondomu wakati wa kujamiiana.
Kupunguza idadi ya wapenzi wa ngono na kuepuka mahusiano ya zinaa yasiyo salama.
Kupima na kutibiwa magonjwa ya zinaa mara kwa mara, hasa kwa wale walio katika hatari kubwa.
Kuepuka kujamiiana na mtu mwenye dalili za maambukizi ya zinaa hadi utakapopata matibabu na kupona kabisa.
Wapi unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu dalili gono?
Pata maelezo zaidi kwa kuwasiliana na daktari wako. Unaweza kusoma makala zingine zinazohusu gono katika linki zifuatazo
Video za makala ya gono
Video ua azuma inatibu gono?
Video ya dawa za kutibu gono
Rejea za mada hii:
Chan PA, et al. Extragenital Infections Caused by Chlamydia trachomatis and Neisseria gonorrhoeae: A Review of the Literature. Infect Dis Obstet Gynecol. 2016;2016:5758387.
Suay-García B, et al. Future Prospects for Neisseria gonorrhoeae Treatment. Antibiotics (Basel). 2018 Jun 15;7(2)
Workowski KA, et al, Centers for Disease Control and Prevention. Sexually transmitted diseases treatment guidelines, 2015. MMWR Recomm Rep. 2015 Jun 05;64(RR-03):1-137.
Unemo M, et al. Antimicrobial resistance in Neisseria gonorrhoeae in the 21st century: past, evolution, and future. Clin Microbiol Rev. 2014 Jul;27(3):587-613.
Unemo M, et al. Antibiotic resistance in Neisseria gonorrhoeae: origin, evolution, and lessons learned for the future. Ann N Y Acad Sci. 2011 Aug;1230:E19-28.
Unemo M. Current and future antimicrobial treatment of gonorrhoea - the rapidly evolving Neisseria gonorrhoeae continues to challenge. BMC Infect Dis. 2015 Aug 21;15:364.
Swanson J. Studies on gonococcus infection. IV. Pili: their role in attachment of gonococci to tissue culture cells. J Exp Med. 1973 Mar 01;137(3):571-89.
Harvey HA, et al. Gonococcal lipooligosaccharide is a ligand for the asialoglycoprotein receptor on human sperm. Mol Microbiol. 2000 Jun;36(5):1059-70.
Edwards JL, et al. A co-operative interaction between Neisseria gonorrhoeae and complement receptor 3 mediates infection of primary cervical epithelial cells. Cell Microbiol. 2002 Sep;4(9):571-84.