Baada ya kutoa mimba, dalili za mimba huendelea kupungua na kuisha kabisa, mabadiliko haya ya dalili huendana na kiwango cha homoni ya ujauzito mwilini yaani bHCG. Homoni bHCG kwa kawaida hupungua kwenye damu kwa jinsi siku zinavyoenda baada ya kutoa mimba. Dalili zote za mimba zinazoonekana hutokana na uwepo wake na endapo homoni hii bado inaongezeka kwenye damu humaanisha mimba bado inaendelea.
Â
Je, inachukua muda gani kwa dalili za mimba kuisha baada ya kutoa mimba?
Kwa kawaida, huchukua siku 2 hadi 14 kwa dalili za mimba kupotea na kuisha kabisa baada ya kutoa mimba, hata hivyo baadhi ya wanwake wanaweza kuendelea kuona dalili ambazo si kali hadi wiki 4 baada ya kutoa mimba kama kuna masalia ya tishu za mimba kwenye kizazi au kama alikuwa na ujauzito wa zabibu. Dalili za chuchu kuvimba na kuuma mara nyingi huchukua muda mrefu kuisha kati ya dalili zote za ujauzito.
Â
Je, Dalili za mimba baada ya kutoa mimba ni zipi?
Dalili za mimba baada ya kutoa mimba zinaweza kuwa katika makundi mawili, yaani dalili za mimba inayoendelea baad ya kutoa mimba, na dalili za mimba iliyoingia baada ya kutoa mimba. Maelezo ya dalili hizo ni kama ifuatavyo:
Â
Dalili za mimba inayoendelea baada ya kutoa mimba
Kama mimba imeshindwa kutoka, dalili za mimba zilizokuwepo awali zitaendelea kuonekana na kuongezeka kwa jinsi homoni bHCG inavyoongezeka kwenye damu. Dalili hizo huwa pamoja na:
Kichefuchefu bila kutapika
Mabadiliko kwenye chuchu
Kukojoa mara kwa mara
Maumivu ya kichwa
Ongezeko la joto la mwili
Hisia za gesi tumboni
Maumivu ya wastani ya nyonga
Uchovu mkali
Kubadilika hali ya hali ya moyo (Hisia)
Kupendelea chakula aina fulani tu
Ongezeko la hisia kwenye harufu
Kuhisi ladha ya umetali
Â
Dalili za mimba mpya baada ya kutoa mimba
Baada ya kutoa mimba, unaweza kushika ujauzito mwingine ndani ya wiki 1 hadi 4 tangu mimba imetoka ikitegemea idadi ya siku katika mzunguko wako hedhi. Mimba ikitungishwa wakati huu hupelekea kuonekana kwa dalili zifuatazo;
Homa wakati wa asubuhi
Kichechefu na kutapika
Kubadilika rangi ya chuchu na kuwa na weusi uliokolea
Kuumwa kwa matiti
Hisia za uchovu
Mwili kulegea
Kukojoa mara kwa mara
Kubadilika kwa hisia ya moyo(kuwa na huzuni au furaha)
Kuvuruga kwa tumbo
Mafua
Maumivu ya kichwa
Kuchagua vyakula
Kukosa hamu ya kula
Hisia ya kizunguzungu
Kuzimia
Dalili zingine zinazoonekana kwa mimba ya zaidi ya mwezi mmoja
Dalili zingine amabazo huonekana baada ya mwezi mmoja kupita ni kama zifuatavyo
Kutoingia mwezini (kutoona damu ya hedhi)
Tumbo Kuongezeka
Hisia za mtoto kucheza tumboni katika wiki ya 16 na kuendele
Kupata haja ngumu
Kubadilika kwa ngozi
Wapi unaweza kupata maelezo Zaidi kuhudu dalili za mimba baada ya kutoa mimba?
Unaweza kupata maelezo Zaidi katika makala ya dalili za mimba katika miezi kwa kubofya linki za Makala zifuatazo.
Â
Rejea za mada hii
Abortion Clinics Amsterdam & Haarlem. After the day treatment or abortion pill. https://www.bloemenhove.nl/en/aftercare/after-the-treatment/#. Imechukuliwa 16.11.2024
van der Lugt B, et al. The disappearance of human chorionic gonadotropin from plasma and urine following induced abortion. Disappearance of HCG after induced abortion. Acta Obstet Gynecol Scand. 1985;64(7):547-52. doi: 10.3109/00016348509156360. PMID: 2417443.
Parents. What to Expect After an Abortion. https://www.parents.com/pregnancy/complications/your-body-after-abortion/#. Imechukuliwa 16.11.2024
ULY CLINIC. Dalili za mimba ya mwezi mmoja. https://www.ulyclinic.com/umri-wa-mimba-kwa-miezi/mimba-ya-mwezi-mmoja. Imechukuliwa 16.11.2024